​Muimbaji nguli wa muziki wa dance, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya pamoja na mwanae, Papii Kocha wameanza maandalizi ya ujio wao mpya, ikiwa ni takriban miaka 14 tangu waachie kibao kipya.

Wawili hao walipewa msamaha na Rais Dkt John Magufuli kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru. Serikali imeonesha nia ya kuwasaidia waimbaji hao wanaopendwa sana kurejea tena kwenye muziki kwa kishindo.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Bi. Juliana Shonza aliwakutanisha na uongozi wa Wanene Studios waliokubali kuchukua jukumu la kuwarudisha tena kwenye muziki. Tayari wameanza kuingia studio kuandaa kazi mpya katika studio hizo kubwa na bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Wameanza kwa kufanya photoshoot, kitu ambacho wamekiri kuwa ni kigeni mno kwao kutokana na kuwa gerezani kwa miaka 14 na wametoka katika nyakati ambazo muziki wa Tanzania umepiga hatua kubwa ukilinganisha na zamani.

“Miaka 14 si mchezo, mambo kama haya si unayaona mwenyewe, niliyamiss, nimemiss vitu vingi, picha za ukweli, mambo haya kule tulipotoka hamna. Lazima uelewe hii ni dunia nyingine,” alisema Papii Kocha wakati wa photoshoot.

Kwa kujiamini, Papii amesema kuwa kazi zao mpya zitakuwa kali zaidi ya zile za zamani. “Kwasababu tumejipanga vizuri na kazi zinazokuja zitakuwa nzuri zaidi ya zile tulizofanya mwanzo,” amesisitiza Papii.

Kwenye photoshoot hiyo iliyofanywa na mpiga picha mahiri Eric Luga, Babu Seya na Papii Kocha walivalishwa na mbunifu wa mavazi, Mtani Nyamakababi.

Unaweza kufuatilia kila hatua ya safari yao kuelekea kuachia kazi mpya kwa kulike ukurasa wao rasmi wa Instagram@babanamwana, Facebook: baba na mwana. Pia subscribe kwenye channel yao ya Youtube iitwayo Baba na Mwana kuona video mbalimbali za behind the scenes.
​​​​​​​​​​​​​​​
Unaweza kuangalia video ya behind the scenes ya upigaji picha kwa kufuata link hii >> https://youtu.be/h-Kdp87now4

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...