THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

bandari ya Dar es salaam yatangazwa kwenye muungano wa falme za kiarabu

Ujumbe wa chama cha wamiliki wa magari ya mizigo pamoja na chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) upo Dubai katika ziara ya kuitangaza bandari ya Dar es salaam kwenye falme za kiarabu (UAE).
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) Bw. Tony Swai nia ya ziara hiyo ni kuipromote Bandari ya Dar es Salaam pamoja na  kukutana na wateja ambao wana-export na ku-import mizigo yao kuja na kutoka Kampala, Uganda.
Mwenyekiti wa wamiliki wa Magari yabebayo Mizigo kutoka Bandari ya Dar Es Salaam Bi. Angelina Ngalula akisalimiana na Balozi Nimisha Madhavan Balozi wa Uganda katika muungano wa  Falme za Kiarabu (UAE) mjini Dubai jana. Kushoto ni Katibu Mkuu chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) Bw. Tony Swai pamoja na Bw. Ordreck Rwabogo mwakilishi wa Mamlaka ya Bandari Uganda na Jimmy Kutosi Mwakilishi wa Uganda Board of Exporters
 Mwenyekiti wa wamiliki wa Magari yabebayo Mizigo kutoka Bandari ya Dar es ealaam Bi. Angelina Ngalula akiongea  na Balozi Nimisha Madhavan Balozi wa Uganda katika Falme za Kiarabu (UAE) mjini Dubai jana. Kushoto ni Katibu Mkuu chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) Bw. Tony Swai pamoja na Bw. Ordreck Rwabogo mwakilishi wa Mamlaka ya Bandari Uganda na Jimmy Kutosi Mwakilishi wa Uganda Board of Exporters