Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe., Ali Hapi, (katikati), akiteremka kutoka juu ya tenki kubwa la kuhifadhia maji linalojengwa huko Mabwepande nje kidogo ya jiji, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya maji wilayani kwake Januari 13, 2018.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU
wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Ali Hapi, amewataka wakandarasi wanaotekeleza
ujenzi wa mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji wilayani
kwake kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo kama ambavyo mkataba unaelekeza.
Mhe.
Hapi aliyasema hayo leo Januari 13, 2018 mwishoni mwa ziara yake ya kukagua maendeleo
ya ujenzi wa miundomnbinu hiyo inayohusisha matenki makubwa manne na vituo vinne
vya kusukuma maji (Booster Stations) ikiwa ni pamoja na utandikaji wa mabomba ya kusafirisha maji.
Mradi
huo ambao unatekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji
Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam, (DAWASA), ni sehemu ya mradi mkubwa wa
uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya
Mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, sehemu ya
mikoa ya Morogoro na Tanga na ulianza kutekelezwa mwezi Machi 2016.
“Mradi
huu ulipaswa kuwa umekamilika Novemba mwaka jana, lakini hatua waliyofikia
baadhi ya maeneo wako asilimia 80, mengine asilimia 75 na mengine asilimia 50,
ahadi yao ni kwamba ndani ya kipindi kifupi kijacho wataweza kukamilisha mradi
huu.” AlisemaMhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi, Mhandisi P.G. Rajani wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa mtambo wa kusukuma maji huko Salasala jijini Dar es Salaam.
Mhe. Hapi, akimsikiliza Mkandarasi, Mhandisi P.G. Rajani(kulia) wa kampuni ya WAPCOS limited ya India, alipotembelea sehemu ya ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji huko Salasala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Modester Mushi kaimu mkurugenzi wa ufundi DAWASA.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...