Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesimikwa rasmi kuwa chifu wa kabila la Wasafwa linalopatikana katika mkoa wa Mbeya .

Dkt. Ndugulile amesimikwa uchifu huo wakati wa ziara yake mkoani Mbeya yenye lengo la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wizara yake imeamua kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii katika ngazi za Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushiriki kwa vitendo kwa kufanya kazi na jamii kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, kilimo, barabara, viwanda na maji, nk.

Ameongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kufuatilia namna ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii ambayo inasisitiza ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini shughuli au miradi ya maendeleo ikiwemo upanuzi na uendelezaji wa miundo mbinu mijini na vijijini kama Shule, Barabara, Zahanati na Maghala kwa kutumia rasilimali zilizopo.

“Niwapongeze kwa kazi nzuri mliyofanya na hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii inayotoa matokeo yenye mashiko na tija katika jamii. Tumieni stadi na mbinu shirikishi kuwezesha maendeleo jumuishi ambapo makundi yote katika jamii yanashiriki katika maendeleo yao” alisistiza Mhe. Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akichanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa boma la madarasa ya shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akipiga plasta kwenye chumba cha madarasa katika ujenzi wa shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akitunukiwa uchifu kutoka kwa Machifu wa Kabila la Wasafwa kama shukurani kwa jitihada za kuamsha ari ya wananchi kujitolea kuchangia shughuli za maendeleo katika ujenzi wa shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo jiji la Mbeya Mkoani Mbeya wakati wa ziara ya yake ya kuamsha ari ya wananchi katika kujitolea kufanya kazi za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akiwa na vazi la kichifu la kabila la Wasafwa pamoja na machifu wengine wa Kabila la Wasafwa wakati alipotunukiwa uchifu wa kabila hilo katika ujenzi wa shule ya Kata ya Mwasanga iliyopo Jiji la Mbeya katika ziara yake ya kuamsha ari ya wananchi wakishiriki kutekeleza utoaji wa haki ya kumwendeleza Mtoto kwa kumpa elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...