Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii, 

Upande wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizoendana na kipato chake  inayomkabili Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai na wenzake watatu umeiEleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi hiyo limepelekwa Takukuru kwa ajili ya upelelezi zaidi.

Wakili wa Serikali Simon Wankyo akisaidiana na wakili Salim Msemo ameeleza leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa upelelezi ikiwa haujakamilika

Wakili Wankyo amedai, jalada la kesi hiyo lilipelekwa kwa  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) kwa ajili ya kusomwa na sasa limerudishwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa ajili ya upelelezi zaidi.Ameongeza, baada ya kukamilisha upelelezi, jalada hilo litarudishwa tena kwa DPP ili kujiridhisha kama maelekezo aliyoyatoa yamefanyiwa Kazi.

Hata hivyo, baada ya maelezo hayo, wakili wa Utetezi Alex Mshumbusi alidai kuwa hategemei upelelezi kuchukua muda mrefu kwa sababu mshtakiwa Gugai alikuwa mtumishi wa Takukuru na tayari alishashtakiwa kinidhamu na Takukuru yenyewe na kupoteza ajira yake.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 31, mwaka huu itakapotajwa.
Mbali na Gugai, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera.Washitakiwa hao wanaokabiliwa na mashitaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.

Katika shitaka la kwanza ambalo ni kumiliki mali ambazo hazina maelezo ambalo linamkabili Gugai, inadaiwa kati ya January 2005 na December 2015, jijini Dar es Salaam, akiwa ofisa wa umma ameajiriwa na TAKUKURU anamiliki mali zenye thamani  zaidi ya Sh 3.6bilioni  ambazo haziendani na kipato chake cha sasa wala cha nyuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...