KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, Doroth Mwanyika amefanya ziara katika Wilaya ya Kilombero, Malinyi na Ulanga  zilizochaguliwa kutekeleza zoezi la upimaji na urasimishaji wa ardhi kwa majaribio katika mkoa wa Morogoro. Lengo kuu likiwa ni kupanga matumizi bora ya ardhi ili kupunguza migogoro na ugomvi baina ya wakulima na wafugaji.

Akihutubia wananchi hao, Katibu mkuu aliwataka wanavijiji hao kutumia fursa mbalimbali zilizo sanjari na mradi wa upimaji na urasimisha ardhi ili kujiletea maendeleao katika ngazi ya familia, Kijiji na taifa kwa ujumla.

Alisema migogoro ya ardhi imekuwa chanzo kikubwa cha kudorora kwa maendeleo maeneo mbalimbali kutokana na muda mwingi kutumika kushughulika kutatua migogoro hiyo na kutumia muda mchache kwenye shughuli za maendeleao.

Katibu Mkuu pia amewashuru wananchi kwa utayari wao wa kumaliza migogoro na kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali ili kujiletea maendeleo yao na Taifa letu. 
AFISA Mipango wa Miji na Vijiji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nickson Mjema akimpatia muhtasari Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Doroth Mwanyika kuhusu elimu na mikakati ya kuwahamasisha na kutoa elimu kwa wna Kijiji wa Nakafulu, wakati wa ziara ya Katibu huyo Wilaya ya Ulanga Mkoa wa Morogoro Januari 10 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, Doroth Mwanyika akijadiliana jambo na mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Jacob Kassema wakati wa ziara yake kwenye Kijiji cha Nakafulu, Wilayani humo Mkoani Morogoro Januari 10, 2018.
MPIMAJI wa Ardhi wa Land Tenure Support Programu (LTSP), Gilbert Utama akimfafanulia Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika jinsi tekinolojia ya mtandao wa simu inavyorahisha upimaji ardhi wakati wa upimaji ardhi kwenye Kijiji cha Ipunguo Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018. Kushoto (kwa katibu Mkuu) ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Jacob Kassema, Katibu Tawala, viongozi wa wizarani na watendaji wa serikali za mtaa wa Mkoa huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika ( wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu wa watendaji wa wizara walipowasili Mlima Ndororo na Mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya kikazi Januari 10, 2018.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika akiongea na kuwapongeza wana Kijiji cha Nakafulu baada kushiriki kwenye mkutano wa hadhara uliolenga kuwapatia elimu na hamasa ya upimaji na urasimisha ardhi katika Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Januari 10 2018.
MMOJA wa wana Kijiji cha Ipungua aliyenufaika na mradi wa Land Tenure Support Programm (LTSP), Yusta Makoto akionesha Kitambulisho chake ambacho hutumika pia na wana vijiji wengine kutambuliwa na kusajiliwa tayari kwa kupatiwa hati za umuliki wa ardhi Mkoani humo.
MMOJA wa wana Kijiji cha Ipungua aliyenufaika na mradi wa Land Tenure Support Programm (LTSP), Dastan Kaweza akionesha pia Kitambulisho chake ambacho hutumika pia na wana vijiji wengine kutambuliwa na kusajiliwa tayari kwa kupatiwa hati za umuliki wa ardhi Mkoani humo.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Doroth Mwanyika (wa nne kulia) na mwenyeji wao, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Jacob Kassema wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu wa watendaji wa wizara walipowasili wilayani hapo Mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kikazi Januari 10, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...