Na Said Mwishehe, Globu ya jamii.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameamua kukutana na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao wanamigogoro mbalimbali ya ardhi kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wake. 

Lukuvi ameamua kutumia siku tatu kuanzia leo hadi keshokutwa kushughulikia migogoro ya ardhi. Hivyo wananchi wenye migogoro ya ardhi wafike Katna Wizara ya Ardhi jijini Dar es Salaam ambako ndiko inafanyika mikutano hiyo. Ambapo ameahidi kusikikiza migogoro yote kwa wale watakaofika kwake. 

Wananchi mbalimbali wenye migogoro ya ardhi ikiwamo viwanja kuvamiwa, kuporwa,kuuzwa bila idhini na malalamiko ya hati kumilikiwa na zaidi ya mtu mmoja, Waziri Lukuvi ametumia nafasi hiyo kutatua mgogoro mmoja baada ya mwingine. 

Kwa leo jumla ya wakazi wa  Dar es  Salaam 250 wamejitokeza kutoa malalamiko yao ya migogoro ya ardhi na anaendelea kuisikiliza . Mmoja ya walitoa malalamiko yao ya mgogoro wa ardhi ni Mohammed Salmin ambaye amesema kuna kiwanja ambacho anayo nyaraka zake lakini kuna mtu mwingine naye anasema ni kiwanja chake na amepewa hati kinyemela. 

"Nimeenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kutoa malalamiko yangu lakini hakuna ambacho kimefanyika. Naomba Waziri unisaidie,"amesema. 

Akijibu hilo Waziri Lukuvi amesema kiwanja hicho kina utata kwani Salmin ameambiwa kiwanja kipo eneo la barabara, "Lakini maofisa ardhi wamempa mtu mwingine hati ya kiwanja hicho kinyemela na kuomba wasaidizi wake kulitafutia ufumbuzi,"amesema Waziri Lukuvi. 

Naye Elhau Medikenya amemwambia Waziri Lukuvi kuwa kuna kiwanja ambacho ni cha mama yake eneo la Tegeta kiwanja namba 279 na anayo hati yake  kimevamiwa.

Amesema mvamizi amejenga nyumba na hataki kutoka, hivyo ameomba waziri kusaidia. Akijibu malalamiko ameahidi kuwa atakwenda mwenyewe kusimamia uboaji wa nyumba ya mvamizi. "Kamwambie huyo ambaye amevamia kiwanja chako kuwa Waziri wa Ardhi atakuja kusimamia kuiboa hii nyumba. Mpe salamu hizo ajue kuwa nitakuja mwenyewe,"amesema Waziri Lukuvi.

Mkazi mwingine Yusufu Azalia amemwambia anacho kiwanja na hati Kinondoni jijini Dar  es Salaam lakini ameshanga imejengwa nyumba ya kifahari na hajui nani amejenga. 

Katika hilo Lukuvi amewaagiza maofisa wake kushughulikia kiwanja hicho ili mwenye hati halisi apewe kiwanja chake na nyumba iondolewe. Wapo baadhi ya wakazi hao wameelezea namna nguvu ya feeha inavyotumika kudhulumu wenye hati halali za viwanja kiasi cha wengine kukamatwa na kufungwa bila sababu za msingi zaidi ya nguvu ya  fedha kupindisha ukweli. 
 Waziri wa  Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliyeshika kipaza sauti akisikiliza kwa makini kero za migogoro ya ardhi kwa wakazi wa Dar es Salaam leo. 
Mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam akitoa malalamiko yake ya ardhi leo jijini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi.
 Sehemu ya wananchi wa Jiji la Dar  es Salaam wakisubiri kutoa kero zao kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  ambaye ameamua kuanzia Leo hadi keshokutwa kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
 Sehemu ya wananchi wa Jiji la Dar  es Salaam wakisubiri kutoa kero zao kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  ambaye ameamua kuanzia Leo hadi keshokutwa kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...