Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yasema kuwa magonjwa yasiyo yakuambukiza yanachangia kiasi kikubwa katika vifo vyote vinavyotokea hapa nchini. 

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa magonjwa yasiyokuwa yakuambukiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Sarah Maongezi wakati akipokea tuzo kutoka kwa TANCDA waliopata mwishoni mwa mwaka huu kutoka katika Shirikisho la Kimataifa la Magonjwa yasiyo yakuambukiza.

“Muongeze juhudi katika kupambana na magonjwa hayo ambayo yanachangia asilimia27 ya vifo vyote hapa Tanzania” Alisema Dkt Maongezi.

Dkt Maongezi aliendelea kusema kwamba Serikali imedhamiria kwa nia kabisa katika kupambana na magonjwa haya kwa kuamua kushirikiana na Asasi mbali mbali nchini ili kutimiza azma hiyo ya kupambana na magonjwa haya.

“Serikali pekee yetu hatuwezi na ndio maana tukashirikiana na Asasi kama TANCDA inayojumuisha vyama vingine kama vile, Taasisi ya Saratani, Taasisi ya Magonjwa ya Moyo, Taasisi ya Mfumo wa Hewa na Taasisi ya Kisukari ambazo kwa ujumla zimejenga ushirikiano katika kupambana na magonjwa haya” Aliongeza Dkt. Maongezi.
Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) katika kikao kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa Hospitari ya Saratani ya Ocean Road kikihusu tuzo ya Elimu kwa jamii waliopata kutoka Shirikisho la kimataifa la magonjwa yasiyo yakuambukiza mwishoni mwa mwaka katika mkutano wa kimataifa uliofanyika katika falme zakiarabu. 
Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akipokea tuzo ya Elimu kwa jamii kutoka kwa Mwenyekiti wa TANCDA Dkt. Tatizo Waane mapema leo katika ukumbi wa Hospitari ya Saratani ya Ocean Road, Wapili kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TANCDA Andrew Swai. 
Kaimu Mkurugenzi magonjwa yasiyo yakuambukiza Dkt. Sarah Maongezi akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo katika picha) katika kikao kilichofanyika mapema leo katika ukumbi wa Hospitari ya Saratani ya Ocean Road kikihusu tuzo ya Elimu kwa jamii waliopata kutoka Shirikisho la kimataifa la magonjwa yasiyo yakuambukiza mwishoni mwa mwaka katika mkutano wa kimataifa uliofanyika katika falme zakiarabu, pembeni yake ni Mwenyekiti wa TANCDA Dkt. Tatizo Waane. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...