Kuanza safari kwa Meli za kisasa za mizigo za MV Njombe na MV Ruvuma ambazo zina uwezo wa kubeba uzito wa tani 1,000 kumefungua fursa za kibiashara kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji.

Meli ya Mv Njombe ambayo imefanya safari yake kwa mara ya kwanza nchini Malawi imefika salama na kutia nanga katika bandari za Nkhata Bay. Meli ya Mv Ruvuma inayopakia shehena ya Clinker inatarajiwa kutia nanga katika Bandari ya Monkey Bay nchini Malawi siku mbili zijazo.MV Njombe ambayo ilibeba takribani tani 800 ya shehena ya saruji kutoka bandari ya Kiwira nchini Tanzania hadi bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi imetia nanga salama na imetumia muda mfupi zaidi kufika Malawi.

MV Ruvuma ambayo ni pacha wa MV Njombe nayo imepakia takribani tani 800 za shehena ya ‘Clinker’ katika bandari ya Kiwira nchini Tanzania kuelekea bandari ya Monkey bay nchini Malawi.Akizungumzia ujio wa shehena hizo za Saruji na ‘Clinker’, Balozi wa Tanzania nchini Malawi ambaye pia alikuja kushuhudia tukio hilo, Mheshimiwa Benedicto Mashiba amesema kwamba kuanza kwa safari hizo ni habari njema kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Malawi .

Balozi Mashiba amesema kwamba, ujio wa meli hizo ni ufunguo wa biashara kati ya Tanzania na Malawi kwani kusafirisha bidhaa kwa njia ya maji ni nafuu na salama zaidi ukilinganisha na barabara.

“Usafiri huu ni mkombozi kwa wananchi na wafanyabiashara wa nchi hizi mbili (Malawi na Tanzania) kwani utawezesha usafirishaji wa mizigo kwa wingi ukilinganisha na njia nyingine kama barabara,” amesema Balozi Mashiba.Mashiba amesema kwamba kuna biashara kubwa ya kusafirisha mizigo kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji kupitia Ziwa Nyasa hivyo kuanza safari kwa meli hizo kutasaidia kuongeza zaidi ukubwa wa shehena katika ya nchi hizo.
 Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba kushoto, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nkhata Bay nchini Malawi Alex Mdooa mara baada ya meli kuwasili bandarini hapo
 Mkuu wa bandari za Ziwa Nyasa, Ajuaye Msese kushoto, akitoa maelezo kwa Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Balozi Benedicto Mashiba kulia, katikati kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkhata Bay nchini Malawi Alex Mdooa
 MV Njombe ilipowasili bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi
MV Njombe mara baada ya kutia nanga bandari ya Nkhata Bay nchini Malawi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...