Na Evance Ng’ingo
MWANAMITINDO wa kimataifa anayefaya  shughuli zake nchini Marekani, Flaviana Matata amekabidhi madarasa mawili kwa shule za msingi iliyopo katika kijiji cha Msinune kata ya Kiwangwa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Flaviana amekabidhi madarasa hayo, baada ya kupewa  jukumu la ulezi wa shule hiyo na wanakijiji wa Msinune mwaka 2014, wakati alipoenda  kuwasaidia wanafunzi mabegi ya shule. majukumju waliyompatai ni pamoja na kuwatengenezea vyoo, ofisi na nyumba za walimu pamoja na kumalizia ujenzi wa darasa 

Tangia alipopewa majukumu hayo alianza kwa ujenzi wa vyoo vya walimu na wanafunzi, na sasa amekabidhi jengo la madarasa kwa darasa la saba na la sita pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule. 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Flaviana alisema, tangia alipopewa jukumu la ulezi wa shule hiyo amekuwa akihangaika huku na kule kupata fedha za kutatua kero za shule hiyo.

Alisema, kwa kufanikiwa kukabidhi jengo hilo la madarasa anaona kuwa ameshiriki kikamilifu katika kutekeleza jukumu lake kama mwanajamii la kusaidia maendeleo ya elimu kwa jamii iliyokuwa na uhitaji mkubwa.

Alisema” sisi kama vijana kama watanzania tunalo jukumu la kujitokeza na kusaidia maendeleo ya elimu na sekta nyingine muhimu nchini kwa kuwa hili sio jukumu la serikali peke yake, sasa nimeshatengeneza vyoo vya walimu na wanafunzi na leo nakabidhi darasa”

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Alex Lugaigalila alisema ujenzi wa darasa huo utawaongezea ufanisi wanafunzi katika masomo yao huku akibainisha wazi ushiriki wa Flaviana kwenye maendeleo ya shule hiyo umeongeza hamasa ya wanafunzi kusoma.

Kwa upande wake Afisa wa elimu wa Kata hiyo,Blasius Alphonce alisema kwa ujenzi wa jengo hilo, Flaviana amesaidia jitihada za serikali katika kuendeleza elimu kwenye kata hiyo yenye vijiji vitano.

Jengo hilo la darasa lililojengwa lina vyumba viwili vikubwa vilivyoezekwa kwa bati huku likuwa na madirisha makubwa yanayowezesha kupitisha hewa na chumba cha mwalimu mkuu.
Mwanamitindo wa Kimataifa afanyae kazi zake nchini Marekani, Flaviana Matata (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo alilojenga la madarasa mawili na ofisi ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Msinune, iliyopo kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana.
Mwanamitindo wa Kimataifa afanyae kazi zake nchini Marekani, Flaviana Matata kushoto akikabidhi mipira kwa wanaafunzi wa shule hiyo, Flaviana ni mlezi wa shule hiyo.
Mwanamitindo Flaviana akionesha cheti cha heshima alichotunukiwa na uongozi wa kata ya Chiwangwa baada ya kuwajengea majengo ya shule.
Flaviana akipokea zawadi ya mbuzi kutokea kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Msinune, Ramadhan Mtokeni (kushoto) huku Diwana wa kata ya Chiwangwa (kulia) Malota Kwagga na Afisa elimu wa kata hiyo Blasius Alphonce kulia kwa diwani na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Msinune, Alex Lugaigalila wakiangalia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...