Na Tiganya Vincent
SERIKALI Mkoani Tabora imeagiza kukamatwa mara moja wazazi au walezi ambao hadi kufikia Jumatatu ijayo (15, January 2018) watakuwa wameshindwa kuhakikisha kuwa watoto wao waliochaguliwa kujiunga Kidato cha kwanza mwaka huu watakuwa hajaripoti katika Shule walizopangiwa.

Agizo hilo limetolewa jana mjini Sikonge na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kupata taarifa kutoka kwa Afisa Elimu Mkoa iliyoakuwa ikionyesha kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza mwaka 2018 bado wengi wao hawajaripoti katika Shule walizopangiwa.

Alisema kuwa kufikia Jumatatu ijayo anataka kupata taarifa na majina ya wanafunzi wote waliochangiwa ambao hawako shuleni ikiwa  na majina ya wazazi wao ili hatua za kisheria dhidi yao ziweze kuchukuliwa kwa kosa la kumkoshesha watoto haki ya kupata elimu.

Mwanri aliongeza kuwa viongozi wa kuanzia mitaa, vitongoji, vijiji , Kata na Wilaya ni vema wahakikishe wanawatafuta watoto wote waliochaguliwa ambao hawako shuleni ili kujua walipo na wanafanya nini kwa kuwa inawezekana wapo ambao tayari wameshaozeshwa.

Alisisitiza kuwa wakikuta mtoto yupo nyumbani na mzazi wake hataki kumpeleka Shule wamukamate mzazi wake ili hawawezi kuwajibika kwa uzembe wake.

“Hapa tutakwenda kwa Sera ya mbanano…kama kiongozi lazima umbane mzazi ambaye hadi hivi sasa hajampeleka mtoto shule wakati wenzake wameshaanza masomo na ikibidi mfikisheni katika vyombo vya Sheria ili ajibu mashitaka yake ya kunyima mtoto haki yake ya elima”alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...