Na Jumbe Ismailly,  SINGIDA   
  
MKURUGENZI wa wanawake wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Salama Masudi amesema kuwa sera ya viwanda nchini haiwezi kufanikiwa iwapo hatutaendana na mabadiliko makubwa ya soko la wakulima na ikiwezekana katika mpango mzima wa mapinduzi ya kilimo wenye lengo la kuwawezesha wakulima wa chini kuelekea soko kuu la dunia kuweza kuinua kipato kutoka kwa wananchi maskini kabisa.

Mkurugenzi huyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida Kaskazini uliofanyika katika Kijiji cha Ughandi, wilaya ya Singida vijijini.

Alifafanua Salama kwamba baada ya wakulima kuwa wamewezeshwa hususani katika maeneo hayo wanayotoka ambapo kilimo ndicho uti wa mgongo,basi kuwezeshwa kwa viwanda hivyo kunawezekana kabisa kutoka maeneo muhimu kulingana na mazao yanayotokana na uwezeshwaji wa viwanda hivyo.

Hata hivyo Salama alisisitiza pia kwamba katika miaka yote wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakipelekewa wagombea wanaume ambao wameshindwa kukidhi haja zao kwa kuwa wanaguswa na matatizo yanayowashika wanawake wenyewe,lakini mwaka huu CUF imewaletea mwanamama huyo mahiri na ambaye wanaamini ndiye suluhisho pekee la matatizo ya wananwake.

“Tunaomba kwa namna ya pekee na utulivu mkubwa tunaomba kura kwa akina mama mtusaidie kuweza kumsaidia mama Delphina Mngazija kwa kuwa ninyi ndio wengi kabisa katika upigaji wa kura na mnatumiwa kuwa chambo cha kuwakandamiza wananchi”alisisitiza Salama.

“Tumewaletea  mama huyo anaguswa na changamoto zinazotukbili sisi wanawake,wengi wetu hapa tunaumizwa na sera mbovu,tumekuja na kampeni pekee  kupitia mgombea wa chama chetu ‘Mwanamke tua ndoo maana yake akiwa sauti ya Bunge kupitia Singida kaskazini anaweza kuongea na serikali kupitia mifuko ya jimbo ili aweze kuleta visima vitakavyosaidia akina mama  kupunguza adha ya maji katika maeneo mnayoishi”alifafanua.
 Wananchi pamoja na wanachama wa CUF wa Kijiji cha Ughandi wakimsubiri kwa hamu Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Prof.Ibrahimu Lipumba kumsikiliza sera za chama na kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Delphina Mngazija.
Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof.Ibrahimu Lipumba (wa kwanza kutoka kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa wanawake wa chama hicho, Salama Masudi kwenye viwanja vya mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Ughandi, wilaya ya Singida Vijijini kabla ya kuongea na wananchi hao.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...