Serikali imepanga kuimarisha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao umo ndani ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili kuzifikia kaya zote masikini nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amesema Bungeni leo wakati akijibu swali kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.

“Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuanza kuandaa sehemu ya pili ya TASAF Awamu ya Tatu ambayo itaendelea kwa miaka mingine mitano” Mhe. Mkuchika amesema na kuongeza Serikali inaelewa yapo maeneo yenye kaya zenye vigezo vya umasikini na uhitaji ambavyo bado havijafikiwa.

Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ulianza mwaka 2013 na unatekelezwa katika Halmashauri 159 za Tanzania Bara, na Unguja na Pemba lakini si katika vijiji, mitaa na shehia zote. 

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA.
TAREHE 31 JANUARI, 2018.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akijibu swali kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini Bungeni leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...