WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ubora wa ujenzi wa kituo cha forodha cha Sirari kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.

Kufuatia hali hiyo amemtaka Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) afike ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma akiwa na mkandarasi aliyejenga kituo hicho.“Serikali haiwezi kuvumilia ujenzi wa hovyo kiasi hiki, namtaka Kamishna wa TRA aje ofisini kwangu Januari 25, 2018 pamoja na mkandarasi aliyejenga kituo hiki akiwa na nyaraka zote za ujenzi wa jengo hilo.”

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Januari 17, 2018) mara baada ya kumaliza kukagua kituo hicho kilichopo wilayani Tarime, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mara.Waziri Mkuu amesema hajaridhishwa na ujenzi huo kwa kuwa upo chini ya kiwango. Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2011 na kukamilika mwaka 2014.

Waziri Mkuu amejionea mwenyewe kuta za jengo hilo zikiwa na nyufa nyingi kuanzia ukutani hadi sakafuni na pia rangi za baadhi ya kuta zikiwa zimebanduka.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wananchi wa wilaya hiyo kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa kuzingatia sheria na wajiepusha na biashara za magendo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimu wagonjwa wakati alipotembela  hospitali ya wilaya ya Tarime akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara, Januari 17, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adm Malima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Sirari na kueleza kutorihishwa kwake na viwango vya ujenzi wa jengo hilo (pichani) ambalo limeanza kuharibika Januari 17, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adama Malima. (Picha na Ofisi  Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Sirari na kueleza kutorihishwa kwake na viwango vya ujenzi wa jengo hilo (pichani) ambalo limeanza kuharibika Januari 17, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya cha Sirari wilayani Tarime Januari 17, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Boreha wilayani Tarime, Januari 17, 2018. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...