WAKAZI wa Kata ya Kinyerezi eneo la Kifuru kwa Kinana wameulalamikia uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kituo cha Tabata jijini Dar es Salaam kwa kitendo cha kutelekeza nguzo na nyaya za mradi wa umeme eneo hilo ambapo zimegeuka kero. 

Wakizungumza jana eneo hilo kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi wakazi hao, wamesema TANESCO kituo cha Tabata walileta nguzo na nyaya tangu mwaka jana na kuziweka barabara inayoelekea King'azi (Kwa Godoro) Mtaa wa Tanganyika ambapo baada ya mvua za mwishoni mwa mwaka jana 2017 baadhi ya nguzo zilianguka na nyaya kutandaa chini jambo ambalo limekuwa kero baada ya kuziba barabara ya mtaa huo na magari kupita kwa taabu.

Mkazi wa Mtaa wa Tanganyika, Rashid Abdallah alisema mradi huo umechukua zaidi ya miaka miwili sasa huku wateja walioomba umeme eneo hilo wamekuwa wakizungushwa kwamba wasubiri mradi huo bila ya mafanikio. 

"...Tumeomba umeme muda mrefu sana tunaambiwa kusubiri mradi lakini mradi ndio kama hivyo wamekuja wamefunga nyaya baada ya mvua kunyesha zimeanguka na wamezitelekeza hapo hapo chini...tunapita kwa shida na wengine kwa hofu maana 
nyaya za umeme zipo chini kabisa si wote wapita njia hazijafungwa umeme sasa hii ni hatari," alisema Mkazi huyo wa Mtaa wa Tanganyika.

Alisema kwa sasa wamekuwa kama walinzi wa nguzo na nyaya hizo za TANESCO mtaani hapo maana wanahofia zikiibiwa huenda matumaini ya mradi huo wanaoahidiwa kila kukicha kukamilika ukatoweka kabisa. "Sasa hivi tumegeuka walinzi maana tunajitahidi haya manyaya yao (waya za TANESCO) waliotelekeza hapo chini baada ya kuanguka yasiibiwe...," alisema Abdallah.
 Gari na pikipiki zikipita kwa shida Mtaa wa Tanganyika, Kifuru Kata ya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, eneo ambalo nyaya na nguzo za mradi wa umeme unaodaiwa kutelekezwa na TANESCO kituo cha Tabata kwa muda sasa baada ya kuangushwa na mvua za mwishoni mwa mwaka 2017.
Baadhi ya nguzo na nyaya za TANESCO Kituo cha Tabata Dar es Salaam zinazodaiwa kutelekezwa na kituo hicho kwa muda sasa baada ya kung'olewa na mvua. Wakazi wa eneo hilo wameilalamikia TANESCO kwa kushindwa kutatua kero hiyo na kukamilisha mradi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...