Na Karama Kenyunko-Globu ya jamii.

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka viongozi wa Serikali na wanasiasa wenye mamlaka ya kikatiba na kisheria kutoingilia muhimili wa Mahakama badala yake waongoze katika misingi yao.

Amesema kumekuwa na uvunjwaji na kudharauliwa kwa amri zinazotolewa na Mahakama  ambayo imepewa mamlaka ya kikatiba ya kutoa haki.Jaji Profesa Juma amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ya wiki ya sheria itakayoanza Januari 27 mwaka huu. 

Amesema,  suala la utoaji haki ni la Mahakama pekee na kwamba viongozi hao wajiepushe kuingilia maeneo yaliyondani ya haki na hadhi ya mamlaka ya kikatiba ya Mahakama.

Amefafanua ibara ya 107A (1) ya Katiba inayozungumzia mamlaka ya utoaji haki inakumbusha kwamba ‘Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Zanzibar,hivyo hakuna chombo cha Serikali wala Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.

 Amesema kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikiwapa taarifa kuhusiana na uvunjwaji wa haki ya kikatiba na kwamba mahakimu ndio wenye hadhi ya kulinda haki hiyo.Amesisitiza kuwa amri zinazotolewa na mahakimu zinavunjwa na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa, hivyo ni wakati wa kuwa kama Bunge ambalo watu wake wanapokiuka taratibu wanachukuliwa hatua.

Amesema, mtu yeyote akajivika nguvu za Mahakama atachukuliwa hatua kwani watakuwa wakali kwa watu wataoingia katika anga za mahakama, na kuomba Katiba ifuatwe na sheria ipewe nguvu na wale wote waliopewa mamlaka wabaki katika maeneo yao, 

Akizungumzia wiki ya sheria, Jaji Profesa Juma ameeleza kuwa maadhimisho ya wiki ya Sheria yataanza Januari 27 hadi 31, mwaka huu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atayazindua  katika viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka  yatakapohitimishwa Februari Mosi ambayo itakuwa ni siku ya Sheria.

Amesema, katika wiki hiyo, kutakuwa na utoaji wa elimu ya sheria na msaada wa kisheria kwa wananchi watakaoshiriki  maadhimisho hayo  kwa kuzifahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mahakama na wadau wa sekta ya sheria.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Juma akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya sheria leo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia tarehe 27 hadi 31,Januari 2018.  Kushoto ni Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Hussein Kattanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...