Na. Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

Serikali kupitia Idara ya Habari ya MAELEZO imesema itatoa kipaumbele kwa waandishi wa habari wa Dodoma kwa kuwapa mafunzo ya kuwajengea uwezo kutokana na mkoa huo kuwa na matukio mengi ya Kitaifa na Kimataifa pamoja na kutembelewa na wageni wa Kimataifa.

Hayo yameelezwa leo mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alipokuwa akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Kanda ya Kati (The Central Press Club (CPC)).

“Nawathibitishia kuwa Serikali sasa iko Dodoma, Dunia sasa inategemea kusikia mambo mengi kutoka Dodoma. Shughuli za Kitaifa na Kimataifa zitakuwa zikifanyika hapa Dodoma ,” alisema Dkt. Abbasi.

Amesema mkoa huo utakuwa unapokea wageni mbalimbali wa Kimataifa hivyo ni lazima waandishi wa habari wa mkoa huo wawe na uelewa wa mambo ya Itifaki na diplomasia ili kuwasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.“Lazima tubadilike hata katika uvaaji wetu, kwani sasa tunaenda kukutana na viongozi wakubwa wa nchi na wa Kimataifa,” aliongeza Dkt. Abbasi.

Aidha amesema, Idara ya Habari MAELEZO itaandaa mafunzo mafupi katika maeneo mbalimbali ya tasnia ya habari ikiwemo masuala ya itifaki na mambo ya diplomasia ili kuwajengea uelewa waandishi hao.Hata hivyo, Dkt. Abbas amesema Idara yake itatafuta ufadhili kwa mabalozi mbalimbali yaliyopo hapa nchini ili waandishi hao wakajifunze namna vyombo vya habari vya Kimataifa vinavyofanya kazi.

“Mwaka 2017 tulifanikiwa kupata ufadhili wa ubalozi wa China na waandishi Kumi walienda China, Bado hatujajua ni waandishi wangapi watafanikiwa kwenda mwaka huu, lakini tutao kipaumbele kwa waandishi wa habari walioko Dodoma,” alisisitiza Dkt. Abbasi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma uliofanyika mapema leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyika mapema leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Edwin Kunambi akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma uliofanyika mapema leo mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...