THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

YANGA ,MWADUI FC KUVAANA KESHO UWANJA WA UHURU

Na Agness Francis-Globu ya jamii

TIMU Soka ya Yanga inatarajia kushuka dimbani kesho kuvaana na timu ya Mwadui Fc katika mchezo wa raundi ya 13 ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Vodavom Tanzania Bara. 

Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam maarufu la Shamba la Bibi.Katika mechi ya raundi ya 12 Yanga walipoteza mchezo wao dhidi ya Mbao FC uliochezwa jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba 

Mabingwa hao watetezi watashuka dimbani huku wakimkosa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Zambia Obrey Chirwa aliyefungiwa mechi tatu na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Pia watamkosa mshambuliaji wao kutoka Zimbabwe Donard Ngoma ambaye bado hajawa fiti. 

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Boniphace Mkwasa amesema maandalizi ni mazuri na wanajua mchezo huo utakuwa mgumu.

“Tumejipanga kupambana kuhakikisha tunashinda mchezo wetu wa kesho,” amesisitiza Mkwasa.