Na Humphrey
Shao , Globu ya Jamii
Ilikuwa Usiku wa February 17 mwaka huu msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Aslay Isihaka alibadilisha historia ya muziki katika Maisha yake kwa kufanya shoo
kubwa ya Mapenzi na Muimbaji Mwenzie Nandy ambae wameshirikiana katika nyimbo
nyingi.
Licha ya
usiku huo kufikiriwa kuwa wa nyimbo za Mahaba mambo yalikwenda tofauti kwa nusu
saa nzima pale Aslaya alipopanda jukwaani na kibao cha “Angekuwepo” wimbo ambao
aliumba kwa ajili ya kumkumbuka Mama yake Mzazi.
Aslay ambaye
aliimba kisha kuishia kati na kwenda kumsogelea Mama Mzazi wa Nandy na kusema
kuwa “natamani muda huu Mama yangu muda huu angekuwa hapa lakini sio mapenzi
yangu...Natamani namimi ningekuwa kama Nandy naimba Mama yangu anaona. Hivyo
nikuombe Mama Nandy kuanzia leo uwe mama yangu hili niweze kupata faraja kama
anayopata mwanao” alisema Aslay.
Maneno yaliteka hisia za watu wengi na kumfanya Mama yake Nandy kuamka na
kwenda kucheza na Aslay na kufanya watu wengi kuinuka kwenda kumwambia
mwanamuziki huyo aendelee kuimba na kuacha kulia.
Aslay ambaye
aliendelea kuimba wimbo huo huku akiwa amekaa chini kwa huzuni na
kutengeneza simanzi kubwa ndani ya ukumbi wa Escape One kwa zaidi ya Dk 30. Wengi walilengwa na machozi na kukubali kuwa Mama ni wa muhimu kuliko kitu
chochote maishani.
Aslay Isihaka akionyesha kidole juu kumshukuru Mungu kwa yote yaliyotekea katika maisha yake.
Aslay akimuomba Mama yake Nandy kuwa Mama yake wa kumlea wakati anaimba wimbo wake angekuwepo
Aslay akicheza na Mama yake Nandy mara baada ya kukubali kuwa Mama Mlezi
Mmoja wa Mashabiki wakinyamazisha Aslay asilie wakati anaimba wimbo angekuwepo
Mashabiki wa muziki wakiwa wamesimama kwa huzuni wakati Aslay akiimba wimbo huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...