Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, jalada la kesi inayomkabili Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai anayedaiwa kuwa na utajiri wa kutisha kwa kumiliki mali zenye thamani ya Sh.bilioni 3 ambazo haziendani na kipato chake limepelekwa (DPP)ili kulipitia na kulitolea uamuzi.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba. Ksi hiyo ilipofika kwa ajili ya kutajwa

Wankyo alieleza awali jalada hilo lilipelekwa kwa DPP ambapo alilipitia na kulirejesha Takukuru na kuelekeza baadhi ya maeneo yafanyiwe uchunguzi zaidi."Maeneo hayo yamekwishafanyiwa kazi na jalada limerejeshwa tena kwa DPP kwa ajili ya kulipitia na kulitolea maamuzi", amesema Wankyo.

Baada ya kudaia hayo aliiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine ili waweze kueleza hali ya upelelezi ikoje.Mshtakiwa Gugai aliiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo kwa siku saba kwani mpaka sasa wamefikisha siku 90 wakiwa wako rumande na upelelezi bado.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 21, mwaka huu, pia ameutaka upande wa mashtaka uhakikishe wanalifanyia kazi jalada hilo kwa kuwa limeanza kuwa zee.Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera

Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.

Gugai na wenzake wanasota mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utak

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...