WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.

Dk Mwigulu amesema yale yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, madawa ya kulevya, na wale wanaotelekeza wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka mahakani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazitatua haraka na kuwarudishia na kuwapa elimu wamekosea wapi.

“Wapeni masomo wamekosea wapi walekezeni na waliowabishi waelekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunawo, tutumie huu mkono wakutatua kwa yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” alisema Dk Mwigulu

Alisema kuwa ipo haja ya vijana sasa kufundishwa zaidi kuhusu sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ya pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila napopita kita vituo vya polisi hukuta pikipiki ni nyingi na makosa yao ni madogomadogo.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba akikagua pikipiki ambazo zimeshikiliwakatika kituo cha polisi pangani. ameagiza polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa mda mrefu na zina makosa madogo waziachie na wasikae nazo kwa mda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...