Mchungaji wa Mji Mtakatifu na kazi nyingine za Palestina na
Jordan Theophilus III, kwa niaba ya wachungaji na viongozi
wote wa Makanisa ya Jerusalemu (Makanisa ya Kigiriki,
Kikatoliki na Kiarmenia),katika hatua ambayo haijawahi
kutokea, Jumapili iliyopita ametangaza kulifunga Kanisa hilo
la Ufufuo lililopo Jerusalemu ya kale hadi itakapotolewa
taarifa nyingine,ikiwa ni kutokukubaliana na kupinga kwao
na sera za utawala wa kivamizi wa Israeli dhidi ya Makanisa
na kuyataka yalipe kodi.
Hayo yamesemwa wakati wa mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika katika kiwanja cha Kanisa hilo la
Ufufuo,ikiwa ni kupinga vitendo vya utawala wa kivamizi
dhidi ya makanisa hayo. Kwani utawala huo hivi karibuni
umeyataka Makanisa hayo ya Jerusalemu yalipe kodi ya mali
ijulikanayo kama"Arnona",yenye thamani ya shekel milioni
kila mwaka, huku ukiingilia mali za Kanisa la Orthodox la
Kirumi kwa lengo hilohilo.
Nao Viongozi wa Makanisa ya Jerusalemu katika mkutano
wa waandishi wa habari, wametoa tamko wakisisitiza ya
kwamba,”Kuyatoza kodi Makanisa mjini Jerusalemu ni
ukiukwaji wa mikataba yote iliyopo na wajibu wa kimataifa
unaodhamini haki za Makanisa na mambo yake maalumu."
Tamko hilo limesisitiza kuwa, hatua hiyo ni "jaribio la
kudhoofisha uwepo wa Kikristo katika jiji hilo," Huku
likionya kuupitisha mpango wa kamati ya wizara iliyo chini
ya utawala wa kivamizi wa Israeli wa kutoza kodi kwa
Makanisa mjini Jerusalemu,ambao unafanyika kupitia
kuchukua kwa nguvu ardhi ya Makanisa hayo yaliyo mjini
hapo.
Serikali ya Palestina imeizingatia hatua ya utawala wa
kivamizi kutoza kodi nyumba za ibada yakiwemo makanisa,
kuwa ni uadui mpya dhidi ya wananchi na maeneo yake
matakatifu, jambo lililopelekea kufungwa kwa kanisa la
Ufufuo lililopo katika mji mkuu unaokaliwa kimabavu. Huku
ukiuchukulia uadui huo mpya kuwa unalenga mji wa
Jerusalemu na taifa letu lote la kiarabu la kipalestina pia
unagusa maeneo yake matakatifu, huku likionya juu ya
madhara makubwa yanayoweza kunyakua ardhi za makanisa.
Serikali imeomba kuingilia kati kwa haraka kwa jumuiya ya
kimataifa ili kusitisha vitendo hivyo vya Israeli, ambavyo
vinahesabiwa kuwa ni mashambulizi mabaya ya
mikataba,makubaliano na desturi zote za kimataifa,
vinavyodhamini uwepo wa uhuru wa kuabudu na kuheshimu
utakatifu wa sehemu za kidini,katika hali yoyote na popote.
Serikali pia imetoa wito maalumu kwa ulimwengu wa kikristo
na kiislamu, wa kuchukua hatua stahiki kwa ngazi zote ili
kuzuia vitendo vya kivamizi, vinavyolenga kwa kiwango sawa
sehemu takatifu za kikristo na kiislamu.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...