Mwimbaji Mahiri wa nyimbo za Kiroho (Injili) Rose Muhando anatarajia kuizindua albamu yake ndani ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2,2018 litafanyika katika uwanja wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu .

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo, amesema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na wanatarajia kuanzia katika jiji La Mwanza ndani ya Uwanja wa CCM-Kiruma Aprili 1, 2018 na kuelekea uwanja wa Halmashauri mjini Simiyu. "Kwa kipindi kirefu Mwimbaji Rose Muhando amekuwa kimya kwa muda mrefu ila kwasasa namtangaza Kinara Rose Muhando ndiyo atakayeongoza jahazi la Tamasha la Pasaka kwa Mwaka 2018 hivyo wananchi mjitokeze kwa Wingi," amesema Msama. 

Aliongeza kuwa mbali na uzinduzi huo, tukio lingine kubwa litakalofanyika ni kuombea nchi amani,hukua kauli mbiu itakuwa "Upendo na Amani "Nipende kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika tamasha la Pasaka ambalo litakuwa la namna yake na waje wajionee vipaji lukuki kutoka ndani ya Tanzania na nje. 
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea maandalizi kabambe ya  Tamasha la pasaka linalotarajia kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2,2018 tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu .
 Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea maandalizi kabambe ya  Tamasha la pasaka linalotarajia kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2,2018 tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...