Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 
 SERIKALI imebaini kwamba maeneo ya bandari, bahari kuu,vituo vya mabasi na viwanja vya ndege  bado yanatumika kupitisha dawa za kulevya nchini. Hata hivyo imeelezwa kuwa wafanyabiashara, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya wameendelea kukamatwa, lengo ni kuhakikisha biashara hiyo inamalizika kabisa. 
Hayo yamesemwa leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akikabidhi gari kwa Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Siyanga. 
 Amefafanua mbali na kukamata meli, pia Serikali imewakamata wasambazaji pamoja na kundi kubwa la wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya sambamba na watumiaji, lengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa salama na kizazi chenye uwezo wa kuzalisha mali. 
 "Serikali imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya na hivi karibuni imekamata meli nyingi, moja ilikiwa inatokea pwani ya Msumbiji na ilikamatiwa maeneo ya Mtwara ikiwa na dawa nyingi za kulevya.
 "Niwakati wa Serikali kuendelea kuiwezesha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na leo hii tunawakabidhi gari hili jipya kabisa ili kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake ipasavyo. 
 "Watanzania wenye tabia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kuacha ikiwa ni pamoja na kazi ya kusambaza, kuzalisha na kutumia na watakaokamatwa wakijihusisha nayo watachukuliwa hatua kali za kisheria,"amesema.
 Ameongeza kwa sasa Serikali inajenga maabara ambayo itatumiwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa dawa wanazozikamata. 
 Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa kushirikiana na Serikali katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa mara wanapowabaini wafanyabiashara, watumiaji na wasambazaji wa dawa hizo. 
Pia wahakikishe wanawalinda vijana ili wasijihusishe na dawa za kulevya. Kwa upande wake Siyanga ameishukuru Serikali kwa kuipatia mamlaka hiyo gari, ambapo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waachane na biashara ya dawa za kulevya.  Pia amesema jamii iache kuwanyanyapaa watu ambao wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya na kushauri kuwa walioathirika na dawa za kulevya wanastahili kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu ya huduma za methadone.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Februari 13, 2018) amekabidhi gari kwa Kamishna Generali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga kwa ajili ya Mamlaka hiyo. Makabidhiao hayo yamefanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...