THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Naibu Waziri awasha Umeme Gongolamboto

Na Zuena Msuya, Dar es salaam 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Gongolamboto chenye uwezo wa MVA 65 na hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar s Salaam, Mgalu alisema Kituo hicho kinapokea umeme kutoka katika mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi katika line ya 132 kV. Mgalu alifafanua kuwa kukamilika kwa kituo hicho kumewezesha uboreshaji wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Kurasini, Kipawa, Kitunda, Chanika na Kisarawe, Ubungo, Mbagala na GongolaMboto.

“Kwa sasa hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika maeneo yaliyokuwa yakisambaziwa umeme kutoka katika kituo hiki haitakuwepo tena, hivyo Serikali itaendelea na juhudi kuwasha umeme katika vituo vingine vilivyosalia,” alisisitiza Mgalu.

Kituo cha Gongolamboto ni miongoni mwa vituo 19 vya kupoza na kusambaza umeme nchini vilivyo katika mradi wa uboreshaji wa vituo hivyo unaofadhiliwa na TEDAP ambapo Jiji la Dar es salaam lina vituo 11, Arusha vituo Sita (6) na Kilimanjaro vituo viwili (2
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyekaa) akiwasha umeme katika kituo cha Gongolamboto kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa njia ya Kompyuta. 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wa pili kushoto) akipata maelezo ya  uendeshaji wa kituo cha Gongolamboto , kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James,(mbele) wakati akikagua mitambo ya kituo hicho kabla ya kuwasha kwa mtambo huo.kushoto ni Kaimu Meneja Miradi , Mhandisi Emmanuel Manirabona. 
Baadhi ya watendaji katika kituo cha Gongolamboto, wakikamilisha kazi kabla ya kuwasha umeme katika kituo hicho. 
Transfoma iliyofungwa mwaka 57, ( kulia) iliyokuwa ikifanya kazi ya kusambaza umeme katika kituo cha Gongolamboto,na mpya zilizowekwa sasa( kushoto). 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, (wapili kushoto) akizungumza na mkandarasi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala. kushoto Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Khalid James