Na Joel Maduka,Geita.

Naibu waziri wa madini Stanslaus Nyongo amewata wachimbaji wadogo wa mgodi wa Nyakafulu na Bingwa kudumisha amani na utulivu katika shughuli zao ikiwemo kujenga desturi ya kufanya usafi wa mazingira ili kuepukana na magojwa ya mlipuko na iwapo hawatazingatia hayo migodi hiyo itafungwa.

Hayo aliyasema wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wachimbaji wadogo kwenye wilaya za Mbongwe na Geita.Alisema ni vyema wachimbaji hao kuzingatia amani na afya zao kwani ndio utaratibu uliowekwa na serikali iwapo ikitokea magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu migodi hiyo itafungwa mara moja.

“Mpo hapa kwa sababu ya kauli ya Mheshimiwa Dkt, John Magufuli lakini vilevile akisikia kwamba hapa hakuna amani na sio wasafi mimi nitatoa amri ya kufunga mgodi huu kwani wizara yangu ndio inahusika kutoa leseni hivyo pamoja na hayo yote amani itawale”alisema Naibu waziri.

Kwa upande wake Rais wa shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini Bw John Bina aliwasisitiza wachimbaji wadogo kujenga desturi ya kulipa kodi ili waweze kuchimba kwa kufata utaratibu, sheria, na kanuni za nchi bila bugudhi yoyote na wagawane kwa utaratibu bila kudhulumiana kwa sababu sehemu wanayochimba kuna leseni ya mtu kwa hiyo wachimbe kwa kuweka akiba ili na wao baadae wakate leseni zao za uchimbaji.

‘’ wachimbaji mmekuwa na tabia ya kula bata na kuhonga pesa zote mnapouza madini acheni tabia hiyo wekeni akiba mkate leseni zenu za uchimbaji zitawasaidia hapo baadae”Alisema Bina.Hata hivyo wachimbaji hao wamemuomba Naibu waziri wa madini Nyongo kuwasaidia kupata leseni ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira yao na vitendea kazi kwa sababu wamekuwa wakitumia njia za asili katika kufanya shughuli zao za uchimbaji.

Naibu waziri wa madini,Staslaus Nyongo amemaliza ziara yake ya siku tatu mkoani Geita,kwa kutembelea migodi mikubwa na midogo huku akisikiliza kero za wachimbaji wadogo na kutatua changamoto ambazo zilikuwa zikiyakabili maeneo hayo. 
Naibu Waziri wa nishati na madini,Stanslaus Nyongo akizungumza na wachimbaji wadogo wa Kijiji cha Nyakafulu wilayani Mbongwe wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Geita. 
Naibu Waziri wa nishati na madini,Stanslaus Nyongo akiwa kwenye shimo ambalo linatumika kuingilia ndani kwaajili ya kuchimba. 
Naibu Waziri wa nishati na madini,Stanslaus Nyongo akizunguka na kukagua baadhi ya maeneo ya mgodi wa Nyakafulu. 
Rais wa shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini nchini Bw John Bina akizungumza na wachimbaji wadogo wa Nyakafulu wilayani Mbongwe. 
Bw,Iddy Mrisho ambaye ni mchimbaji akielezea masikitiko yake na namna ambavyo wamekuwa wakinyanyasika kutoka kwa viongozi wa vikundi. 
Baadhi ya wachimbaji wadogo wakimsikiliza Naibu waziri wa madini,Staslaus Nyongo. 
Wachimbaji wadogo wakiwa wamebeba mabango ambayo yanamalalamiko

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...