Na Ripota Wetu, Arusha

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amepata ajali ya gari katika eneo la Mdori mkoani Manyara.

Taarifa kuhusu tukio hilo zinadai kuwa Kamanda Mkumbo amepata ajali leo, baada ya gari aliyokuwa akiitumia kupasuka gurudumu la nyuma.

Baada ya kupasuka kwa gurudumu hilo, gari ilipoteza muelekeo na kisha kupinduka.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Yusuph Ilembo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Ambapo amesema ndani ya gari hiyo kulikuwa na watu watatu akiwamo Msaidizi wa Kamanda Mkumbo pamoja na dereva wake na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.

Ilembo amesema ajali hiyo imetokea leo saa nane mchana wakati Kamanda Mkumbuko akiwa njiani kutokea mkoani Singida kwenda Arusha na alipofika eneo la katikati ya Mdori na Minjingu ndipo guruduma la nyuma upande wa kushoto la gari hiyo lilipasuka na kusababisha ajali hiyo.

Amesema Kamanda Mkumbo ameumia kidole chake cha shahada na baada ya ajali hiyo amepelekwa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Arusha ambako anaendelea na matibabu wakati dereva wake naye analalamika maumivu kwenye paja la upande wa kushoto na msaidizi wake anasema hajaumia kwani hasikii maumivu mahali popote.

Amewataka wananchi wa Arusha kutokuwa na hofu kwani Kamanda Mkumbo hali yake inaendelea vema na kubwa ni kumuombea ili arudi kwenye hali yake ya kawaida na kuendelea na majukumu mengine ya kulitumikia Taifa.
Baadhi ya Wananchi wakishuhudia tukio a ajali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...