Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kufanya mapitio na ukaguzi wa zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma katika Halmashauri zao.
Lengo la maelekezo hayo ni kujiridhisha na sifa za watumishi waliojiriwa kwa cheti cha darasa la saba na walioajiriwa kwa sifa ya cheti cha ufaulu wa Kidato cha Nne kama wamewasilisha vyeti vyao na kuhakikiwa.Dkt. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo katika kikao kazi na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe.
Dkt. Ndumbaro ametoa angalizo kwa  Makatibu Tawala wa Mikoa  nchini kuhakikisha wanawaondoa katika Utumishi wa Umma watumishi ambao hawajawasilisha vyeti vya Kidato cha Nne kwa ajili ya uhakiki na wale waliodanganya kuwa ni darasa la saba ili kukwepa zoezi la uhakiki wa vyeti vya kidato cha Nne,Sita na Ualimu.
Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa, ofisi yake itatoa Waraka wa kuzitaka Mamlaka za Sekretarieti za Mikoa kwenda kufanya ukaguzi katika Halmashauri zao ili kujiridhisha na namna zoezi la uhakiki liliyofanyika.
Katibu Mkuu Dkt. Ndumbaro katika kikao kazi hicho amepokea changamoto mbalimbali na kuzitolea ufafanuzi ili kuleta mabadiliko ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma nchini.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaroakizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya  Mkoa wa Njombe katika kikao kazi na waumishi hao chenye lengo la  kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi.
 Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika kikao kazi na watumishi hao chenye lengo kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi.
Mmoja wa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe akiwasilisha hoja yake kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati wa  kikao kazi na watumishi hao chenye lengo kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi hao na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi. 
 
Imetolewa na James Katubuka Mwanamyoto
Afisa Habari
Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...