*Baadhi ya matumizi hayatawezekana kwa sababu za kisheria

Na Said Mwishehe,Globu wa Jamii

SERIKALI imesema imepokea bajeti ya gharama ya mazishi ya aliyekuwa Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha Usafirishaji (NIT) Aqwilina Akwiline(pichani enzi za uhai wake) ya Sh 80,150,000 kutoka kwa familia huku ikieleza baadhi ya matumizi hayatakubaliwa kwani kisheria hayagharamiwi na Serikali.

Pia imesema kwenye makisio hayo kuna gharama zilizokuwa zimepewa makadirio ya juu.Hivyo Serikali kupitia Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia jana jioni imekaa na familia ili kuondoa changamoto hiyo na hatimaye kupata bajeti ya pamoja.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mwasu Sware imesema Wizara hiyo kupitia kwa Katibu Mkuu wake  Dk.Leonard Akwilapo ilipokea makisio ya gharama za mazishi kiasi hayo kutoka kwa Msemaji wa familia hiyo Festo Kavishe. 
"Kumekuwepo na taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha makisio ya gharama za mazishi ya Aqwilina Akwiline. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaufahamisha umma kuwa bajeti hiyo inayosambaa kwenye mitandao ni makadirio yaliyoandaliwa na familia ya marehemu.
"Baada ya kupokea makisio hayo Katibu Mkuu Dk.Akwilapo alitahadharisha kuna baadhi ya matumizi hayatakubaliwa kwa kuwa kisheria hayagharamiwi na Serikali . Pia katika makisio hayo kuna gharama ambazo zilikuwa na makadirio ya juu,"amesema.
Amesema kutokana na hali hiyo Dk.Akwilapo aliagiza kuwe na kikao kati ya Wizara na ndugu wa marehemu ili kuweka sawa changamoto hizo ili kuwa na bajeti ya pamoja. Hivyo kikao kilifanyika jana jioni na kufikia muafaka.
"Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa taratibu nyingine za 
mazishi zinaendelea vizuri,"amesema Sware.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...