THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

serikali yatakiwa kuzitambua kazi za wanawake katika mipango ya Taifa

NA VICENT MACHA - DAR ES SALAAM.

SERIKALI imetakiwa kuzitambua kazi za kutoa huduma zinazotekelezwa na wanawake na kuziingiza katika Mipango ya Taifa kwani zinaweza kusaidia kuongeza pato la Taifa.

Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia (TGNP) Bi. Lilian Liundi alipokuwa akitoa Mhuktasari wa Kongamano la Wanawake na Uongozi.

Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika siku ya jumanne ya tarehe 27 Mlimani City jijini Dar es salaam, likihudhuriwa na wanawake mbalimbali walio katika nafasi za uongozi na waliostaafu.Mkurugenzi huyo alisema kuwa kuna haja ya serikali kuzitambua shughuli mbalimbali zinazotolewa na wanawake kama huduma kwa lengo la kujipatia kipato kwani uchunguzi umebaini kuwa wanawake hutumia muda wa masaa 10 mpaka 15 kwa siku kwa shughuli hizo hivyo wanakosa muda wa kufanya shughuli za kujipatia kipato.

Aidha Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa lengo kuu la Kongamano hilo ni wanawake kwa pamoja kuweza kujadili namna gani wataweza kuongeza nafasi za uongozi na maamuzi kwani bado hawajaweza kufikia lengo ambalo ni 50 kwa 50.

Lakini pia kuweza kusherekea, kupongezana na kuajadili changamoto mbalimbali anazokutana nazo mwanamke katika Nyanja ya elimu, afya na umiliki wa ardhi swala ambalo bado ni changamoto kubwa kwa wanawake wengi hivi sasa. Bi. Lilian aliendelea kusema kuwa kutakuwa na kuenzi na kukumbuka mchango uliotolewa na wanawake ambao walikuwa katika ngazi za uongozi maamuzi kuanzia ngazi ya jamii mpaka taifa.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri msataafu Mama Marry Nagu, lakini pia kutakuwa na wadau zaidi ya 250 wanawake kwa wanaume viongozi wa sasa na wastaafu katika kuhakikisha kongamano hilo linaleta tija kwa jamii yetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo jijini Dar es salaam katika mkutano na waandishi kuhusu kongamano la Wanawake Uongozi. 
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi wa katikati akiwa na jopo la wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika kuandaa Kongamano la Wanawake na Uongozi. 
Waandishi wa habari wakiendelea na kazi yao.