Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuisaidia Tanzania kutokana na mchango mkubwa wa kuwahudumia wakimbizi ambao imekuwa ikiutoa kabla na baada ya uhuru, licha ya uchumi mdogo ilio nao. 
Waziri Mahiga ametoa wito huo leo Jijini Dar Es Salaam katika kikao cha Baraza la Wakimbizi Duniani (World Refugees Council-WRF) kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia jana kwenye Hoteli ya Hyatt Regecy, Kilimanjaro.

Waziri Mahiga alieleza kuwa Tanzania ilipokea wakimbizi kutoka Poland wakati wa vita ya pili ya dunia na mwaka 1959 ilipokea wakimbizi kutoka nchi ya Rwanda. Aidha, baada ya uhuru, Tanzania imekuwa ikipokea wakimbizi mara kwa mara na wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Tanzania ilipokea wakimbizi wengi zaidi duniani.
Aliendelea kueleza kuwa athari zinazotokana na kupokea wakimbizi wengi ni nyingi na kubwa hivyo, ni jukumu la Jumuiya ya Kimataifa kuzisaidia nchi zenye wakimbizi wengi, hususan zile zenya uchumi mdogo.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari kuhusu dhamira ya kuanzishwa kwa Baraza la Wakimbizi Duniani ambalo yeye ni Mwenyekiti Mwenza. Kushoto kwake ni  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa Tanzania kujitoa katika Mpango wa kutafuta suluhu ya kudumu ya tatizo la wakimbizi duniani.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika kikao cha Baraza la Wakimbizi Duniani kinachofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini DAr es salaam.
Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...