Na estom sanga - katavi.

Tatizo lililokuwa linaukabili mkoa wa Katavi la watoto kutoka katika kaya maskini kuacha masomo na kutafuta vibarua kwenye migodi ya machimbo ya madini,limepungua kwa kiwango kikubwa baada ya kuanza kutekelezwa kwa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bibi. Lilian Charles Matinga amesema hayo mwishoni mwa wiki alipofungua Warsha ya Wandishi wa Habari wa mkoa wa Katavi juu ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini .

Bi.Matinga amesema kupungua kwa tatizo la ajira ya Watoto kumetokana na moja ya masharti ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaohimiza watoto kuhudhuria masomo kwa zaidi ya asilimia 80 kwa mwezi ili waweze kupata huduma za Mpango.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amesema walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, wameanza kuboresha maisha kwa kujenga nyumba za kudumu huku wengine wakijiongezea kipato kwa kuanzisha biashara ndogo ndogo kama ufugaji wa kuku,bata, nguruwe na wengine kukuza shughuli za kilimo.

Ili miradi ya Walengwa hao wa TASAF iweze kupata mafanikio yanayotarajiwa ,Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza Wataalam wa ugani kuweka mipango ya kuwatembelea walengwa na kuona namna ya kuwasaidia kuboresha miradi wanayoianzisha.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Mtaalamu wa Mawasiliano wa TASAF,Bi. Zuhura Mdungi amesema baada ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kufikia takribani miaka minne sasa , katika maeneo mengi ya utekelezaji wa Mpango ,walengwa wameboresha maisha yao huku kukuwa na mafanikio makubwa katika nyanja za elimu, afya na uanzishaji wa miradi midogo midogo ya kiuchumi. 
Mkuu wa wilaya ya Mpanda ,Bi.Lilian Charles Matinga (aliyesimama) akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya waandishi wa habari juu ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Katavi. Kulia kwake na Mtaalamu wa Mawasiliano wa TASAF,Bi. Zuhurua Mdungi na kushoto kwake ni Mratibu wa TASAF wa mkoa wa Katavi .
Mtaalamu wa Mawasiliano wa TASAF,Bi. Zuhura Mdungi (aliyesimama) akitoa mada kwenye warsha ya waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF mkoani Katavi.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa mkoa wa Katavi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Mpanda Bi. Lilian Charles Matinga (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha juu ya kuwajengea uelewa wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Moja ya nyumba zilizojengwa na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwa kutumia ruzuku wanayopata kutoka TASAF katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...