Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imewafundisha soka timu ya MultiChoice Tanzania (DSTV) baada ya kushinda katika mchezo maalum wa ‘Media Day’ uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam.
Taswa FC ilianza mchezo huo kwa ‘dharau’ na kujikuta ikipachikwa bao katika dakika ya tatu ya mchezo. Bao hilo liliwashtua timu hiyo ya waandishi wa habari na kusawazisha katika dakika 11 kupitia kwa Hare Temba baada ya pasi safi ya Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.
Bao hilo liliwaduwaza DSTV iliyokuwa ikiongozwa na  Meneja Uhusiano wake, Johnson Mshana ambaye pamoja na kung’ara, walijikuta wakipachikwa bao la pili kupitia kwa Wilbert Molandi kufuatia mpira wa kona wa Majuto. DSTV ilisawazisha katika dakika za mwisho wa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili ilikuwa cha ‘kiama’ kwa DSTV baada ya kupachikwa bao la tatu na Majuto kufuatia mpira wa faulo nje ya eneo la hatari.
Baada ya bao hilo, DSTV walinyong’onyea na kupachikwa mabao matatu yaliyofungwa na Zahoro Mlanzi baada ya pasi safi  kutoka kwa Saidi Seif na Ibrahim “Maestro” Masoud.
Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Johnson Mshana alisema kuwa  mbali ya matokeo hayo, lakini lengo lao limefanikiwa kwa kuweza kuwakutanisha waandishi wa habari za michezowa vyombo mbalimbali kwa kushirikiana na timu ya Taswa FC.
“Lengo la kukutana ni kufurahi pamoja ikiwa ni kucheza, kula na kunywa baada ya kazi kubwa ya kuendeleza gurudumu la maendeleo, waandishi wamekuwa na ushirikiano mzuri na sisi katika shughuli mbalimbali,” alisema Mshana.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary aliipongeza MultiChoice Tanzania kwa kuandaa halfa hiyo ambayo iliwakutanisha waandishi wa habari si chini ya 250.
“Ni faraja kwetu kujumuika hapa, mara ya kwanza tulikutana katika ukumbi wa Nyambizi na kujadiliana masuala mbalimbali, japo tulikuwa wachache, hapa wigo umeongezeka na tunaamini tutakuwa tukifanya hafla kama hizi mara kwa mara,nawashukuru sana,” alisema Majuto.
 Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC, katika picha ya pamoja na  timu ya MultiChoice Tanzania (DSTV) kabla ya mchezo wao maalum wa ‘Media Day’ uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
Mpambano kati ya Taswa FC na  MultiChoice Tanzania (DSTV) katika  mchezo wao maalum wa ‘Media Day’ uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...