Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

TUME Usuluhishi na Uamuzi (CMA) imetoa tuzo kwa aliyekuwa Meneja wa kiwanda cha Konyagi David Mgwassa (pichani juu kulia) ya kulipwa dola za Kimarekani 200, 000 ndani ya siku 14 kuanzia leo kama gharama za usumbufu baada ya kuachishwa kazi isivyo halali na Kampuni ya Tanzania Brewaries (TBL).
Pia  TBL inatakiwa kumlipa Mgwassa Sh.milioni 412   kama fidia ya kusitishwa kwa haki zake  na pia ilipe mkopo wa gari lenye thamani ya  Sh.milioni 94 ambalo lilikopwa na Mgwasa akiwa kazini.

Uamuzi huo umetolewa na Mwamuzi, Bw. Alfred Massay katika shauri la mgogoro wa kazi  lenye kumbukumbu namba CMA/DSM/ILALA/R.49/16,   ambapo Mgwassa alifungua madai mbalimbali dhidi ya TBL,  Sabmiller Africa na Sabmiller PLC-London. 
Mgwassa pamoja na mambo mengine mbali mbali, alikuwa akilalamikia kuachishwa kazi isivyo halali na kuomba alipwe mishahara ya miezi 36 kama fidia na pamoja na malipo ya bonasi kwa miezi mitatu ambayo ni sawa na zaidi ya Sh.milioni 261.5.
Mgwassa aliajiriwa na TBL kati ya Februari mwaka 1982 na Juni mwaka  2015 na katika kipindi cha kusitishwa kwa mkataba wake wa ajira alikuwa akiilipwa mshahara wa Sh. 17,191,451.88 kwa mwezi. Hata hivyo, ajira kati ya TBL na Mgwassa ilifikia mwisho Juni 25 mwaka  2015 baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya mkataba wa kustaafu mapema.

Baada ya uamuzi huo kutolewa,Mgwassa aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili Alex Mshumbusi alisema ameridhishwa na uamuzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...