Na Leandra Gabriel,Globu ya Jamii

IDARA ya Uhamiaji nchini inawashikilia watanzania 9, ambao ni  wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala(KIU) jijini Dar  es Saalam kwa madai ya kuzuia maofisa wa idara yao kutofanya kazi yao walipofika chuoni hapo.

Akizungumza na Michuzi Blog, leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa  Idara ya Uhamiaji Ally Mtanda amesema watu hao tisa wamekamatwa  jana kwa tuhuma za kuzuia maofisa wa idara hiyo wasitimize  majukumu yao na kwa sasa wanawahoji. 

"Watu hao baada ya maofisa wetu jana kufika pale KIU waliamua kuwazuia kwa kufunga milango ili tusipate nafasi ya kufanya kile ambacho kimetupeleka,"amesema.

Hivyo kukamatwa kwa watu hao kunafanya idadi ya wanaowashikiliwa na Idara ya Uhamiaji kufikia 48."Idara ya Uhamiaji inaendelea kuwahoji na kati ya hao wanaoshikiliwa wapo raia wa Nigeria watano, raia wa Congo mmoja, raia wa Uganda 30, raia wa Kenya 3 pamoja na hao raia wa Tanzania 9,"amesema.

Amefafanua Idara ya Uhamiaji itaendelea kukagua vyuo mbalimbali  nchini kwani ni agizo la Wizara ya Elimu, Sayansi na  Teknolojia. Alipoulizwa kwanini wameanza na KIU amejibu huo ni  mwanzo tu kwani watapita kwenye maeneo mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...