Kama kawaida maneno kama “kinuklia” au “mionzi” yanatisha ikiwa yanatumika katika nyanja za afya na maisha marefu. Hata hivyo, haiwezekani kufikiria utibabu za siku hizi bila ya teknolojia mpya inayotumia radioisotopu za kinuklia.

Duniani watu wanajua juu ya utumiaji wa mionzi na radioisotopu katika utibabu hasa kwa ajili ya utambuzi na utibabu ya magonjwa magumu mbali mbali. Katika nchi zilizoendelea, ambapo robo ya watu wote wa dunia wanaishi, mtu mmoja wa watu watano anatumia utibabu za utambuzi za kinuklia kila mwaka.Lakini swali muhimu ni vipi dawa za kinuklia na radioisotopu (dawa zenye mionzi) zinafanya kazi na vipi zinaweza kuleta faida kwa Watanzania?
Kwanza, mionzi ni ufungaji wa nishati tu. 

Kama taa ya mwanga atomu za mionzi zinazalisha nishati inayotumika kwa ajili ya utibabu. Dawa za mionzi zinaingizwa katika mwili wa mgonjwa na sindano, kwa kumeza au kwa kuvuta pumzi.Ukubwa wa mionzi unaotumiwa ni mdogo sana. Mwilini radioisotopu zinatoa vyembe fupi (alpha au beta) ambavyo vinapoteza nishati yao yote katika umbali mfupi sana, kwa hivyo vinaathiri sana seli zilizoharibiwa. Kwa ujumla dawa za mionzi zinatumika kama matibabu: uharibifu wa seli za kansa, upungufu wa maumivu ya kansa ya mifupa na arthritis.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...