Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha 

Wakulima wa zao la korosho Mkoa wa Pwani wamefanikiwa kupata kiasi cha sh. bilioni 57.7 kutokana na mauzo ya zao la korosho ,msimu huu. Mafanikio hayo yametokana na mfumo wa stakabadhi ghalani ambao umetumika miaka mitatu iliyopita tangu kuanzishwa kwenye Mkoani hapo. 

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC). Alisema fedha hizo zimepatikana kutokana na minada sita hadi kufikia Januari mwaka huu ambapo minada hiyo ilianza Novemba mwaka jana. 

Ndikilo alifafanua ,kilo zilizouzwa ni 20,399,325 za daraja la kwanza ni kilo 11,554,380 na daraja la pili ni kilo 8,814,945. “Kilo hizo kwa daraja la kwanza ziliingiza kiasi cha shilingi bilioni 35.8 na daraja la pili shilingi bilioni 21.4 kwa wakulima wa mkoa huo” 

“Wilaya ya Mkuranga imeweza kuongoza kwa kuuza na kupata mapato makubwa ikiwa imeingiza kiasi cha bilioni 13 ikiwa imeuza kilo milioni 4.1, Kibiti waliingiza bilioni 4 kwa kuuza kilo milioni 4,Rufiji bilioni 2.8 kwa kuuza kilo milioni 1.5,” alisema Ndikilo. Awali katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji Shangwe Twamala alieleza, bei ya juu kwa korosho daraja la kwanza ilikuwa ni shilingi 3,817 kwa kilo na daraja la pili ni shilingi 2,950. 
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na wajumbe wa kikao cha ushauri cha mkoa huo (RCC)kuhusiana na mipango na mkakati mbalimbali ya kuendeleza maendeleo ya kimkoa.(Picha na Mwamvua Mwinyi) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...