VICTOR MASANGU, KISARAWE 

WANAFUNZI wapatao 472 na walimu zaidi ya 25 katika shule ya sekondari Makulunge iliyopo katika kata ya kiluvya Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani kwa sasa wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo UTI,na kipindu pindu kutokana na vyoo ambavyo wanavitumia kwa sasa vipo katika mazingira hatarishi na miundombinu yake kuwa mibovu hivyo wakati mwingine inawalazimu kwenda kujisaidia katika maeneo mengine.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ambayo imefanyika katika kata ya Kiluvya na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ambapo baada ya kutembelea shule hiyo ya sekondari ameweza kubaini kuwepo kwa mapungufu makubwa ya walimu wa shule hiyo kutokuwa na choo chao hivyo kuchangia na wanafunzi wao.

Wakizungumza kwa masikitiko wanafunzi hao akiwemo Waziri Mwinjuma na Zuwena Mohamed wamebainisha kwamba kwa sasa wanapata shida kubwa sana kutokana na kuwepo kwa mazingira magumu ya miundombinu ya vyoo na kwamba kunahatarisha usalama wa afya zao kutoka na kukithiri kwa uchafu pamoja na miundimbinu kuwa mibovu na baadhi ya vyoo hazina milango na sehemu za ukuta zimeanza kubomoka.

Walisema kuwa kwa sasa kutokana na kuwepo kwa hali hiyo baadhi ya wanafunzi wengine hususan wa kike wanapata ugonjwa wa UTI kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi ukilinganisha na matundu ya vyoo yaliyopo hivyo wakati mwingine wanafunzi kujisaidia sehemu ambayo sio salama kabisa.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya sekondari Makulunge iliyopo kata ya kiluvuya katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea shule na kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Waziri wan chi Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo akizungumza na viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa ziaara yake ya kikazi aliyoifanya katika kaata ya Kiluvya kwa ajili ya kujionea shughuli mbali mbali za kimaendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
Mmoja wa walimu wa shule ya sekondari Makuunge Ester Matemu akizungumza kuhusiana na changamoto ambayo ianwakabili ya ukosefu wa vyoo,(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...