THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAZIRI MKUCHIKA AKUTANA NA UJUMBE WA DfID

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) ameishukuru Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) kwa kuwa moja kati ya wadau wa maendeleo nchini.

Mhe. Mkuchika amesema hayo leo katika kikao na ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) kilichofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Ninapenda kuishukuru DfID pamoja na Serikali ya Uingereza kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kuleta maendeleo kwa Watanzania wote.

Mhe. Mkuchika amesema DfID kama moja ya washirika wa maendeleo wamechangia kwa kiasi kikubwa jitihada za serikali za kupambana na rushwa, na moja ya matokeo yake ni kuongeza uwajibikaji katika utoaji huduma kwa wananchi na kuondosha rushwa kupungua.

Mhe. Mkuchika ameuhakikishia ujumbe wa DfID kuwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iko tayari muda wowote kushirikiana na DfID katika kuleta maendeleo.Kiongozi wa DfID nchini, Bi. Beth Arthy ameahidi kuendeleza ushirikiano katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiwa katika kikao na ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, (hawapo pichani) ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) akiwa katika kikao na ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. 
Kiongozi wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, Bi. Beth Arthy akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) hayupo pichani wakati wa kikao leo jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa ujumbe kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID) nchini Tanzania, Bw. Nicholas Leader akiwa katika kikao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) hayupo pichani, ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.