CHANGAMOTO ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Jiji la Mwanza kuwa historia baada ya Serikali kuanza utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa miwili ya maji yenye thamani ya sh. bilioni 112.
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jumanne Februari 20, 2018 wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Halmashauri za Jiji la Mwanza, Ilemela na Nyamagana akiwa katika siku ya sita  ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.
Waziri Mkuu amesema miradi hiyo inahusisha kuboresha upatikanaji wa maji katika maeneo ya pembezoni wenye thamani ya sh. bilioni 75 ambao utahusisha ujenzi wa chanzo kipya cha maji kwenye eneo la Butimba chenye uwezo wa kutoa lita milioni 40 kwa siku. 
Ametaja maeneo yatakayonufaika na mradi huo kuwa ni Butimba, Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Sawa, Lwanhima, Kishiri, Nyahingi, Luchelele, Malimbe, Bulale, Fumagila, Usagara, Kisesa, Buswelu, Nyamwilolelwa, Kahama, Nyamadoke, Nyamhongolo, Mondo, Kiseke, Kangae, Meko, Nsumba na Bulola. 
Waziri Mkuu amesema mradi mwingine ni wa kuboresha upatikanaji wa maji katika maeneo ya milimani wenye thamani ya sh. bilioni 37 ambao ulianza kutekelezwa Februari, 2017 na unatarajiwa kukamilika Agosti 2018. 
Amesema wakazi 105,649 wanaoishi katika maeneo ya milimani hususan yaliyo juu ya matenki ya maji ambayo hayapati huduma kwa sasa watanufaika. Maeneo hayo ni Nyasaka, Bugarika, Nyegezi, Capripoint, Mjimwema, Nyakabungo na Kitangiri. 
Amesema Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao. 
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka viongozi na watendaji wa Jiji la Mwanza kuhakikisha wanashirikiana katika kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi wa dini, kabila wala kipato. Pia amewataka watambue miiko na ukomo wa madaraka yao. 
Amesema watumishi hao wanatakiwa wawe waaminifu na wasimamie vizuri matumizi ya fedha za uetekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye maeneo yao na wahakikishe zinatumika katika miradi husika kama ilivyoelekezwa na Serikali. 
Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Bw. Kiomoni Kibamba kuifuta Taasisi ya Bunge la Jamii kwa sababu inakiuka sharia na kazi inazofanya zinalingana na za bunge. Taasisi hiyo ilisajiliwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiakata utepe wakati alipoweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mbarika – Misasi katika  kijiji cha Manawa  wilayani Misungwi, Februari 19, 2018. Wapili kulia  ni mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga na wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa  wa Mwanza, John Mongella. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mbarika- Misasi katika kijiji cha Manawa wilayani Misungwi Februari 19, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella na wapili kulia ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kiwanga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua  madarasa yanayojengwa kwa nguvu za wananchi katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi Februari 19, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, wapili kulia ni Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga na watatu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubi mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi, Februari 19, 2018. 
  Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Misungwi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamayinza, Februari 19, 2018.
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyamayinza wilayani Misungwi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadahara kijijini  hapo,  Februari 19, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la pamba lenye ukubwa w hekari 6 la  Bw. Muhoja Ngole (kulia kwa Waziri Mkuu) katika kijiji cha Mondo wilayani Misungwi, Februari 19, 2018.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...