WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa azindua Mpango Mkakati wa Afya Moja na Dawati la Kuratibu Afya Moja nchini ni  lenyelengo  katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa mahala safi na salama kwa kuishi na kufanya kazi za kimaendeleo.kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama.na kushoto ni Waziri wa kilimo kutoka serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hamadi Rashid Uzinduzi hou umefanyika leo Februari 13 /2018 jijini Dar es salaam   
Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa mahala salama na penye afya bora huku akielezea jitihada zinazochukuliwa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na matukio hatarishi kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam, wakati anazindua Mpango Mkakati wa Afya Moja na Dawati la Kuratibu Afya Moja nchini huku akisisitiza uzinduzi huo ni muhimu hasa kupindi hiki ambacho kumekuwepo na muingiliano mkubwa kati ya binadamu, wanyama na mazingira.

Amesema dhana ya dhana ya Afya Moja inafaa kutumika zaidi katika nchi zinazoendelea kwani inatoa fursa kwa wadau mbalimbali kushirikana katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

"Mpango huu wa Afya Moja ni ajenda ambayo ipo kwenye nchi mbalimbali duniani na kwa Tanzania ni mpango ambao tunaamini utasaidia kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yatokanayo na binadamu, wanyama na mazingira,"amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Ameongeza mkakati wa kukabiliana na maradhi yatokanayo na wanyama na mazingira ni muhimu kwa nchi nyingi za Afrika kwani zipo kwenye hatari zaidi.

Amesema katika Bara la Afrika kuna maeneo mengi yenye mapori makubwa ,hivyo ni rahisi kuwepo kwa magonjwa ya kuambukizwa yanayotokana na binadamu, wanyama na mazingira,hivyo Afya Moja imekuja wakati sahihi.

Ametoa mfano wa mapori makubwa yaliyopo kwenye Bonde la Mto Kongo, ambalo mazingira yake yamekuwa ni kitovu cha magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola, Homa ya Bonde la Ufa (RVF), Marburg na mengineyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...