THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Archive for March 2018

HOTUBA YA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA 19 MARCH 2018


ISACA TANZANIA CHAPTER WORKSHOP: UNDERSTANDING COBIT 5 IMPLEMENTATION ESSENTIALSNEWS ALERTRais Magufuli kuwaapisha Mabalozi Wateule wawili kesho Ikulu Dar es SalaamBODABODA KUANZA KUTUMIKA KUSAFIRISHA MAKOZI YA TB

*Ummy Mwalimu azindua dawa ya TB kwa watoto,aagiza wanafunzi nao kupimwa ugonjwa huo 

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema wapo kwenye mchakato wa kuingia mkataba na waendesha bodaboda ili watumike kusafirisha makozi ya Kifua Kikuu(TB) kutoka vituo vya afya kwenda Hospitali kwa ajili ya vipimo.

Pia amezindua rasmi dawa ya TB kwa ajili ya watoto wenye kubainika kuwa na ugojwa huo ambayo ni tamu na ina ladha ya matunda huku akisisitiza umuhimu wa kila mmoja wetu kupambana kutokomeza TB kwani ni janga la kitaifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa watalaam na wadau wa afya na hasa katika ugonjwa wa TB, Waziri Ummy Mwalimu amesema ugonjwa huo ni tishio nchini na duniani kwa ujumla.

Hivyo amesema kuna jitihada mbalimbali ambazo zinafanywa na  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya  Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Amesema licha ya kufanikiwa kuwatambua wagonjwa wa TB lakini changamoto kubwa bado wengi wao wanajificha.Hivyo inakuwa ngumu kutambua na ubaya wake TB inaambukizwa kwa hewa.
Amesema takwimu zinaonesha mgonjwa wa TB anaweza kuambukiza watu wengine 20, hivyo kazi inayofanyika sasa ni kuendelea kuelimisha jamii kupima ili kubaini iwapo wana TB au laa.

Pia amesema kutokana na uhaba wa vifaa vya kupima wenye ugonjwa wa TB inalazimu kwenye vitio vya afya baada ya kuchukua makozi ya mtu anayedhaniwa kuwa na ugonjwa huo husafirishwa kwa gari hadi hospitalini.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungungumza wakati wa mkutano wa wadau wa afya waliokuwa wanajadili namna ya kutokomeza Kifua Kikuu(TB) ambapo ametumia mkutano huo kuzindua dawa ya TB kwa watoto waliobainika na watakaobainika kuwa na ugonjwa huo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa ufafanuzi kabla ya kumpatia dawa ya TB mtoto Salome Makulusi(3) aliyebainika kuwa na ugonjwa huo.Waziri Mwalim amesema dawa ya TB tayari imeingia nchini na leo ameizundua rasmi wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhammed Bakari Kambi.
 Baadhi ya wadau wa afya hasa wanaojihusisha na tiba ya ugonjwa wa TB wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI WA UJENZI WA NYUMBA 36 ZA JESHI LA POLISI MFIKIWA CHAKE CHAKE PEMBA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. 
kuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akihutubia mara baada ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akipokea mifuko ya saruji zaidi ya elfu sita kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Tanga Cement Bw.  Lawrence  Masha jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


WAUZA DAWA ZA KULEVYA KUNYONGWA MAREKANI

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii.

RAIS wa Marekani Donald Trump ameeleza mpango wake wa kupambana na wauzaji wa dawa za kulevya chini humo.

Akihutubia huko Manchester, Trump amesema kuwa dawa za kulevya yanagharimu maisha ya watu wengi kutokana na matumizi ya dawa na wanaosababisha vifo hivyo hupewa adhabu ya muda mfupi.

Amefafanua na tayari Bunge limetenga kiasi cha dola za Marekani bilioni sita kwa ajili ya kupambana na tatizo hilo.

Ameeleza lazima kuwe na umakini na kuelekeza adhabu kali sambamba na ile ya kifo kwa wauzaji wa madawa ya kulevya.

Ifahamike katika kampeni zake za urais Trump alitoa ahadi nzito zikiwemo kujenga ukuta ili kudhibiti wahamiaji haramu,  kutengua mpango wa afya wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Obama Barrack na ile ya  Marekani kwanza.


WATUHUMIWA WIWILI WA UJAMBAZI WAUAWA WAKIJIBIZANA RISASI NA POLISI

Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

JESHI la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema watu wawili wanaotuhumiwa ni majambazi wameuawa wakati wakijibizana kwa risasi na Polisi.

Pia limesema limekamata silaha mbili AK 47 zenye namba UB38341997 na risasi 17 ndani ya magazine na AK47 1967TY4577 na risasi 24 ndani ya magazine pamoja na pembe za ndovu vipande 9 katika pori la Makerema wilayani Kasulu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Maltin Otieno leo kuwa Machi 19 mwaka huu, tano usiku kwenye pori la Makere katika Kijiji cha makere wilayani Kasulu watu wawili ambao ni Norbert Andrew na Bukuru Stiven ambaye ni mkimbizi kambi ya Nyarugu waliuawa kwa kushambuliwa na majambazi wenzao wakati wakienda kuwaonesha Polisi silaha ambazo walikuwa wamezificha porini.
Amesema watu hao walikamatwa katika tukio moja la kuvunja kibanda na kuiba na mmoja wa majambazi hao waliangusha simu eneo la tukio iliyowezesha polisi kumkamata.
"Baada ya kuhojiwa na polisi waliwataka wenzao na kufanikiwa kuwakamata wanne.Katika mahojiano walikiri kuhusika na matukio mauaji, na uvamizi katika nyumba za watu wilayani hapo.

"Hata hivyo baada ya mahojiano hayo mtuhumiwa aliwaongoza Polisi mpaka kambi ya Nyarugusu na kufanikisha kukamatwa mtuhumiwa mwingine na baada ya kupekuliwa alikutwa na silaha walizokuwa wakizitumia kufanya uhalifu,"amesema.Amesema baada ya kukutwa na silaha hizo alieleza kuna silaha nyingine tano amezificha porini,hivyo polisi waliondoka na watuhumiwa hao na walipofika maeneo ambayo wameficha silaha ndipo risasi zilianza kupigwa na majambazi wenzao.

Amesema hali hiyo ilisababisha askari kulala chini na watuhumiwa hao ambapo watu hao watuhumiwa hao wa ujambazi walifariki dunia. Aidha Kamanda Otieno amewaomba wakimbizi wote wenye silaha katika kambi za wakimbizi kuzisalimisha polisi kabla ya Machi mwishoni na baada ya hapo watanza msako kupitia kamati ya ulinzi na usalama na mkoa huo.

Wakati huohuo Solomoni Ntihazo kwa kosa la kukutwa na pembe za ndovu vipande tisa ambapo vipande viwili ni vikubwa na vipande saba ni vidogo.


DC KIBAHA AZINDUA CHUO CHA VETA KUWASAIDIA VIJANA WA VIJIJINI

KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na uchumi wa viwanda  hatimaye  kanisa la Mission to Unreached Area Church (MUAC) lililopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani limeamua kujenga chuo cha ufundi stadi (VETA) kwa lengo la kuwawezesha  vijana wanaotoka katika maeneo ya vijijini ili waweze kujifunza fani mbali mbali ambazo zitawasaidia kupata ujuzi na kuanzisha viwanda vidogovidogo na kujiajiri wao wenyewe.

Kauli hiyo ilitolewa na  Askofu mkuu  wa kanisa la Mission to Unreached Area (MUAC), Samwel Meena wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa chuo hicho ambazo zimehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini, serikali pamoja na wageni kutoka nchini Ujerumani ambao wanajiusisha na masuala ya kuwasaidia vijana kuwainua  kiuchumi kupitia makanisa.

Askofu huyo alibainisha  kuwa lengo kubwa la kuanzisha chuo hicho ni kutokana na kubaini kuwepo kwa wimbi kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana hususan wale wanaoishi vijijini na kujikuta wanashinda kutwa nzima bila ya kujishughulisha na kazi yoyote , hivyo ana imani  kuwepo kwa chuo hicho ni moja na ukombozi mkubwa ambao utaweza  kuwasaidia kuondokana na hali ngumu ya kimaisha na kuondokana na dhana ya kuwa tegemezi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza jambo wakati wa halfa ya uzinduzi rasmi wa chuo cha ufundi stadi (VETA) kilichojengwa na kanisa la Mission to Unreached Area Church (MUAC) lililopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
 Askofu mkuu wa kanisa la Mission to Unreached Area (MUAC),  Samwel Meena kulia akimpa maelezo mafupi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama wakati wa halfa ya ufunguzi wa chuo hicho cha VETA.
Askofu mkuu wa kanisa la Mission to Unreached Area (MUAC), Samwel Meena akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa chuo hicho cha ufundi stadi amabcho imejngwa kwa ajili ya kuweza kuwasaidia vijana wanaotoka katika maeneo ya vijiji.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


MFANYABIASHARA APANDISHWA MAHAKAMA YA KISUTU KWA KUSAFIRISHA GRAMU 214 DAWA ZA KULEVYA


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mfanyabiashara, Hariri Mohammed Hariri (45), mkazi wa Kinondoni, amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu Tuhuma za kusafirisha zaidi ya gramu 214 za dawa za kulevya.

 Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Clara Chalwe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi imedaiwa Machi 2 mwaka huu huko Kinondoni Matitu ndani ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa alisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 214.11.

 Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chohote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevy isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Na imeahirishwa hadi Aprili 4 mwaka huu


SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA WATAIFA WA UBORESHAJI WA HUDUMA YA UPASUAJI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI ya kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  imezindua mpango wa taifa wa kuboresha huduma upasuaji ambayo kila mtu anaweza kumudu  kufikia 2025.

Akizungumza wakati wa uzinduaji wa mpango huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki amesema kuwa mpango huo umekuja wakati mwafaka kutokana na sera ya afya miaka mitano kuisha hivyo mpango huo kuingia katika sera ya miaka mitano.

Dk. Mpoki amesema kuwa mpango huo uko katika muda mwafaka kutokana na hatua mbalimbali za uboreshaji afya kwa wananchi katika upatikaji wa huduma za upasuaji hali ambayo itaokoa maisha pamoja na kuongeza uzalishaji.

“Upasuaji salama ni ishara ya  kila mtanzania anaweza kupata huduma za afya na kuongeza uzalishaji  ,kuboresha huduma za upasuaji bora pamoja na dawa za usingizi ni muendelezo wa kuboresha afya ya uzazi kwa nchi nzima” amesema Dk.Mpoki.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa taifa wa huduma ya upasuaji, jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Shirika la GE, Asha Varghese akizungumza kuhusiana na Tanzania kupokea mpango wa upasuaji na kuingiza katika mpango wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasioambukiza, Dk. Sarah Maongezi akizungumza hali ya upasuaji nchini, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki akikata utepe kuashiria uzinduzi mpango wa taifa kuboresha huduma za upasuaji, jijini Dar es Salaam.
Sehemu wataalam wa afya  wa nchi mbalimbali wanaoshiriki mkutano wa afya unaofanyika nchini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Muhimbili Yapokea Msaada wa Vitanda na Magodoro

 Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vitanda 14, magodoro 12  pamoja na drip stands kutoka Australia Tanzania Society ambavyo vitasaida kuimarisha utoaji wa huduma hospitalini  hapo.

Akipokea msada huo jijini Dar es Salaam  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt.  Juliethi Magandi amesema kwa muda mrefu hospitali imekua na ushirikiano na tasisi hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo kufanya  upasuaji wa ubingwa wa juu.

“Kipekee nichukue fursa hii kuwashukuru rafiki zetu hawa Australia Tanzania Society kwa msaada huu  walioutoa kwani tumekua tukishirikiana kwa zaidi ya miaka mitatu sasa,”.  amesema Dkt. Magandi.

Amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina jumla ya vitanda 1,507 na kwamba kina mama wajawazito na watoto pekee wanatumia karibu  ya nusu ya vitanda hivyo.  “Hivyo  msaada huo umekuja wakati muafaka  kwani hospitali bado ina mahitaji kutokana na kutoa huduma zake kila siku kwa saa 24,”.
 Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Julieth Magandi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla kukabidhiwa vitanda 14 na magodoro 12 ambayo yametolewa na Australia Tanzania Society. Kulia ni Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
 Muuguzi Alice Msonda na Velena Joahackim wakitandika kitanda baada ya kukabidhiwa vitanda na magodoro na Australia Tanzania Society.
 Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi vitanda 14 leo. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akizungumza na waandishi wa habari leo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


WAZIRI MKUU ATAKA SULUHISHO LA MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa za Afrika kutoa mapendekezo ya namna ya kutokomeza magonjwa yasiyo ambukiza kwa wakuu wa nchi hizo ili yafanyiwe kazi.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumatatu, Machi 19, 2018) wakati akifungua Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya kutoka nchi tisa wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA-HC)

Alisema magonjwa yasiyo ambukiza ni miongoni mwa magonjwa ambayo yameendelea kuwatesa wananchi kwa kiasi kikubwa katika nchi nyingi za Bara la Afrika, hivyo vema mawaziri hao wakatoa mapendekezo ya namna ya kuyatokomeza.Waziri Mkuu alisema magonjwa hayo yanaweza kudhibitiwa kwa kuhamasisha wananchi kuboresha lishe na kusisitiza ulaji wa vyakula bora, kufanya mazoezi na kubadili mitindo ya maisha.

“Magonjwa yasiyoambukiza yanaongoza kwa kusababisha vifo katika baadhi ya nchi wanachama wa ECSA. Magonjwa haya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya mfumo wetu wa lishe na maisha, hivyo ni muhimu suala hili likatafutiwa ufumbuzi.”

Waziri Mkuu alisema magonjwa yasiyoambukiza pamoja na magonjwa mengine ya milipuko kama ebola, homa ya bonde la ufa, dengue, homa ya manjano yamekuwa kikwazo cha maendeleo kwa katika baadhi ya nchi.

Pia, Waziri Mkuu aliongeza kuwa sekta ya afya ni muhimu kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya nchi zote zikiwemo zilizoendelea na zinazoendelea, hivyo changamoto zote zinazoikabili zinapaswa zipewe kipaumbele katika utatuzi.Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu alisema malengo ya mkutano huo ni kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazohusu sekta ya Afya na kuyapatia ufumbuzi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mawaziri wa Afya kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afya kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ambazo ni Tanzania, Malawi, Lethoto, Uganda, Kenya, Rwanda, Zambia, Zimbabwe na Muwakilishi kutoka nchini Mauritious.Pia Katibu wa jumuiya hiyo Profesa Yoswa Dambisya, Muwakilishi wa Benki ya Dunia Dkt. Paolo Belli pamoja na wadau wa sekta ya afya kutoka nchi hizo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MACHI 20, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Afya wa Uganda .Sarah Opendi ,wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) kushoto ni Wazri wa Afya wa Malawi Atupele Muluzi,Waziri Mkuu amefungua mkutano huo jana March 19, 2018 Jijini Dar es salaam.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua wa Mkutano wa 65 wa Baraza la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Africa (ESCA Health Community) 
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


TAZAMA SHEREHE ZA MKOMAULA KABILA LA WAYAO MKOANI RUVUMA

Kulia ni Sultani Mataka ambaye ni sultani wa tano wa kabila la wayao Tanzania akisalimiana na Mwandishi wa Ruvuma TV Nancy Mbogoro .
………………….
Kupitia kipindi cha Utalii cha Talii na Ruvuma TV tumekuandalia kipindi maalum kinachohusu Sherehe za asili za kabila la Wayao katika mkoa wa Ruvuma, Sherehe hizi zinakwenda kwa jina la Mkomaula, Sherehe hizi hufanyika kila mwaka na kuongozwa na Sultan Mataka ambaye ni Sultan wa tano wa kabila la Wayao Tanzania. Hii hapa chini Video yake.


DC MTWARA AFUNGUA KONGAMANO LA WAJASIRIAMALI MJINI MTWARA

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda akifungua kongamano la wajasiriamali katika ukumbi wa chuo cha ualimu Mtwara lililofadhiliwa na shirika la VSO. Lengo la kongamano hilo ni kuwajengea wajasiriamali hao uwezo na utayari wa kukamata fursa zitakazotokana na ugunduzi wa gesi unaoendelea katika mkoa huo na ukanda wa mikoa ya kusini kwa ujumla wake Kongamano hilo limefanyika leo 20.3.2018.
Wawasiliamali hao wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Mtwara Evod Mmanda hayupo pichani wakati akifungua kongamano la kuwajengea uwezo linalofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu mjini Mtwara. 
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda akiwa katika picha ya pamoja na wajasiriamali hao mara baada ya kufungua kongamano hilo mjini Twara leo.


KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YAKAGUA UJENZI WA OFISI ZA UHAMIAJI MKOANI MTWARA.

 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu (kushoto) akisalimiana na afisa uhamiaji Mkoa wa Mtwara, James Mwanjotile (kulia) wakati kamati hiyo ilipoenda kukagua ujenzi wa ofisi za uhamiaji Mkoa wa Mtwara tarehe 19 Machi, 2018 Mkoani Mtwara.
 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu (kulia) akipokelewa na katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) wakati kamati hiyo ilipoenda kukagua ujenzi wa ofisi za uhamiaji Mkoa wa Mtwara tarehe 19 Machi, 2018 Mkoani Mtwara.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Mussa Zungu (katikati) akisisitiza jambo pale kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa ofisi za uhamiaji Mkoa wa Mtwara tarehe 19 Machi, 2018 Mkoani Mtwara.
 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama wakimsikiliza kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara (hayupo kwenye picha) akizungumza wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje, ulinzi na usalama, Mhe. Salum Rehani akizungumza jambo wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa katika kikao kilichofanyika  ofisini kwake Mkoani Mtwara.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)


TAFITI MBALIMBALI ZILIZOFANYWA NA WIZARA YA HABARI KUWASILISHWA KWA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA

Na Genofeva Matemu - WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kufikisha taarifa ya hatua ambayo Tanzania imefikia katika harakati za kutafiti na kuhifadhi kumbukumbu za ukombozi wa Bara la Afrika kwa mawaziri wa utamaduni wa nchi za kusini mwa Afrika ili nchi hizo wanachama ziweze kuendelea na hatua nyingine ya kuchangia katika ujenzi wa kituo cha kuhifadhi kumbukumbu hizo.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo Mkoani Mbeya alipofanya ziara kukagua maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kusema kuwa serikali ipo katika mpango ambao maeneo yaliyotumika katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika yatakarabati na kurejesha muonekano wake wa awali ili yasipotezi historia.
“Majengo yaliyotumika katika harakati za urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika ni sehemu ya historia na maeneo muhimu sana ambayo yanatakiwa kuboreshwa ili yaweze kuendelea kuwepo katika muonekano ule ule wa awali kwa lengo la kutokupoteza historia yake” amesema Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali imechukua wajibu wake wa kubaini maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kuwaomba viongozi wote nchi nzima kuendelea kubaini maeneo na vitu vilivyotumika katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika vilivyopo katika maeneo yao ili wizara   iyaendeleze kwa maslahi ya taifa na Afrika kwa ujumla.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika (kulia) wakati wa ziara yake leo Mkoani Mbeya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto mwenye miwani) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika (kulia mwenye miwani ) alipotembelea eneo la Game lililotumika kama kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji leo Mkoani Mbeya wakati wa ziara yake kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika
Nyumba zilizopo katika eneo la Game zilizotumiwa na wapigania uhuru wa Msumbiji ambazo kwa sasa zinatumiwa na Idara ya Maliasili na utalii.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma (kulia) alipotembelea Nyumba ya Binti Matola aliyekuwa mwanaharakati na rafiki wa Mwalimu Nyerere ambaye aliweza kumhifadhi Hayati Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wakati wa ziara yake kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Mkoani Mbeya.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 2827

*Ni baada ya kupatikana na hatia ya makosa 419 likiwemo la utakatishaji fedha

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mfanyabiashara Stanley Mwaura kutumikia kifungo cha miaka miaka 2827 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa 419 ikiwemo utakatishaji  fedha.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kumaliza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Shaidi amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake  15 waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi, wamethibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo.

Katika kesi hiyo mshtakiwa alijitetea mwenyewe.

Hakimu Shaidi amesema,  mshtakiwa huyo ana makosa 419, ambapo kosa la 1 hadi 99 ni kughushi, kosa la 100 hadi 198 ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kosa la 199 hadi 297 kujipatia nyaraka kwa njia ya uongo.  Huku kosa la 298 hadi 396 ni utakatishaji fedha na kosa la 397 hadi 419 ni kughushi.

Hakimu Shaidi amesema kuwa katika kosa la 1 hadi 99 Mahakama inamuhukumu mshtakiwa Murithi kwenda jela miaka 7 kwa kila kosa.

Katika kosa la 100 hadi 198 la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu Mahakama inamuhukumu kwenda jela miaka 7 kwa kila kosa.

Pia kosa la 199 hadi 297 mshtakiwa anahukumiwa kwenda jela miaka 7 kwa kila kosa.

Katika kosa la 298 hadi 396 mshtakiwa amehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni 100 kwa kila kosa sawa na Sh.bilioni 9.9 ama kutumikia kifungo cha miaka miaka 6 gerezani kwa kila kosa.

Pia kosa la 397 hadi 419 amehukumiwa kwenda jela miaka 7 kwa kila kosa.

"Mahakama imekutia hatiani katika makosa hayo 419 ambapo unahukumiwa kwenda jela miaka 7 kwa kila kosa ambapo jumla itakuwa miaka 2827 lakini adhabu hii itaenda sambamba ambapo utatumikia miaka 7 tu gerezani," amesema Hakimu Shaidi.

Miongoni mwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili mshtakiwa ni utakatishaji fedha ambapo inadaiwa kati ya February 6 na 7,mwaka 2012 maeneo ya Jiji la Dar es Salaam alijihusisha katika muamala wa kuhamisha fedha ambazo ni Sh.Mil 4.9 kinyume na sheria.

Pia inadaiwa kati ya April 30 na Mai 5, mwaka 2013 alihamisha kiasi cha Sh.milioni 6.5 kinyume na sheria.


UCSAF YAPEWA SIKU 14 KUWASILISHA RIPOTI YA HALI YA MAWASILIANO PEMBA

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameupa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wiki mbili kwenda Pemba kukagua hali ya mawasiliano ya simu za mkononi na kuwasilisha taarifa hiyo ofisini kwake.
Mhandisi Nditiye ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Zanzibar ya kukagua hali ya mawasiliano kisiwani humo na kutembelea taasisi za mawasiliano zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambapo suala la mawasiliano ni la muungano.
Nditiye amesema kuwa amepokea taarifa kutoka kwa wabunge wa Kisiwa cha Zanzibar kuwa hali ya mawasiliano kwenye kisiwa hicho sio nzuri na sehemu nyingine hakuna mawasiliano licha ya kuwa kuna minara ambayo inatoa huduma za mawasiliano ila kutokana na jiografia ya Pemba ambapo kuna milima na mabonde hivyo mawasiliano si ya uhakika. “Nawaagiza muende Pemba mkaainishe maeneo yote ambayo hayana mawasiliano na muwasilishe taarifa hiyo ofisini kwangu baada ya wiki mbili,” amesema Mhandisi Nditiye.
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisi ya Zanzibar Bi. Esuvatie-Aisa Masinga wakati akiwasilisha taarifa yake kwa Mhandisi Nditiye kuhusu majukumu ya ofisi yake ya usimamimizi na udhibiti wa mawasiliano na posta, amekiri kuwa yapo baadhi ya maeneo Pemba na Unguja ambapo hali ya mawasiliano sio nzuri na hairidhishi.
 Meneja Ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Zanzibar, Bi. Esuvatie-Aisa Masinga akitoa taarifa ya hali ya mawasiliano Zanzibar kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara yake kisiwani humo
 Meneja Msaidizi Mtandao wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Zanzibar Bwana Mohamedi Ali Haji akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) njia yanakopita mawasiliano kutoka Dares Salaam kuja Zanzibar wakati wa ziara yake kisiwani humo
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ( wa kwanza kulia) akisikiliza kwa makini maelezo kutok akwa mfanyakazi wa TTCL kuhusu mwitikio wa wateja kwa huduma zinazotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakati wa ziara yake Zanzibar
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akitoa maelekezo kwa mwakilishi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bwana John Munkondya kuhusu vituo vya mawasiliano vilivyopo Zanzibar wakati wa ziara yake kisiwani humo.
 Mfanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Zanzibar, Bwana Khalfan Mmkahirika akimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano namna scanner inavyofanya kazi ya kukagua mizigo na vifurushi vinavyosafirishwa na Shirika hilo ndani na nje ya nchi ili kulinda usalama wa raia na taifa wakati wa ziara yake Zanzibar. Mwenye koti nyeusi ni Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika hilo Bwana Hassan Mwang’ombe.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ziara yake kwa taasisi za mawasiliano Zanzibar. Kushoto ni Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika hilo Bwana Hassan Mwang’ombe na kulia ni Mkurugenzi wa Huduma wa Shirika la Simu Tanzania (TTCL) Bwana Hussein Selemani Nguvu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA