Na Veronica Simba – Dodoma
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa wito kwa wadau wote wa sekta ya madini nchini, kuzingatia sheria mpya ya madini ambayo inaelekeza namna bora ya usimamizi wa sekta hiyo.
Alitoa wito huo jana, Machi 22 mwaka huu kwa nyakati tofauti, alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Dodoma, kukagua shughuli mbalimbali za madini.
 “Moja ya mambo muhimu ambayo sheria mpya ya madini inaelekeza ni kutunza rekodi za uzalishaji wa madini ili Serikali iweze kujua ni kitu gani kinazalishwa na hatimaye tuweze kujua kodi gani zinalipwa na wenye leseni husika,” alifafanua.
Aidha, Naibu Waziri aliwataka wenye leseni kushirikiana na wachimbaji wadogo wa madini ili waweze kunufaika kupitia kazi wanazofanya. “Kwa maneno mengine, asitokee mtu wa kumnyanyasa mchimbaji mdogo eti kwa sababu tu ana leseni,” alisisitiza.
Akizungumza na wamiliki wa leseni pamoja na wachimbaji wadogo wa madini wa dhahabu katika eneo la Nholi wilayani Bahi, Naibu Waziri alipongeza uamuzi wao wa kuanzisha kampeni ifikapo Aprili mwaka huu, kupanda miti kwenye maeneo yao ili kurejesha hali nzuri ya mazingira.
Vilevile, aliwaagiza kuweka wigo kuzunguka mashimo yaliyo wazi ili kuonyesha hali ya tahadhari kuwa eneo hilo ni hatari na linaweza kusababisha ajali, ikiwa ni hatua mojawapo ya kuzingatia usalama migodini.
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, akizungumza na wananchi wa Nholi wilayani Bahi, kulipo na machimbo ya madini ya dhahabu, alipowatembelea Machi 22 mwaka huu, kujionea shughuli wanazofanya.
 Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili kutoka kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Halmashauri, wakati wa ziara yake kukagua shughuli za uchimbaji dhahabu katika eneo la Nholi, Wilaya ya Bahi, Machi 22 mwaka huu. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Kitundu.
 Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Dodoma, Silimu Mtigile (kulia) akifafanua jambo kwa wananchi wa Kijiji cha Nholi wilayani Bahi, wanaojishughulisha na uchimbaji wa dhahabu; wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto), Machi 22 mwaka huu

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...