KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na uchumi wa viwanda  hatimaye  kanisa la Mission to Unreached Area Church (MUAC) lililopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani limeamua kujenga chuo cha ufundi stadi (VETA) kwa lengo la kuwawezesha  vijana wanaotoka katika maeneo ya vijijini ili waweze kujifunza fani mbali mbali ambazo zitawasaidia kupata ujuzi na kuanzisha viwanda vidogovidogo na kujiajiri wao wenyewe.

Kauli hiyo ilitolewa na  Askofu mkuu  wa kanisa la Mission to Unreached Area (MUAC), Samwel Meena wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa chuo hicho ambazo zimehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini, serikali pamoja na wageni kutoka nchini Ujerumani ambao wanajiusisha na masuala ya kuwasaidia vijana kuwainua  kiuchumi kupitia makanisa.

Askofu huyo alibainisha  kuwa lengo kubwa la kuanzisha chuo hicho ni kutokana na kubaini kuwepo kwa wimbi kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana hususan wale wanaoishi vijijini na kujikuta wanashinda kutwa nzima bila ya kujishughulisha na kazi yoyote , hivyo ana imani  kuwepo kwa chuo hicho ni moja na ukombozi mkubwa ambao utaweza  kuwasaidia kuondokana na hali ngumu ya kimaisha na kuondokana na dhana ya kuwa tegemezi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza jambo wakati wa halfa ya uzinduzi rasmi wa chuo cha ufundi stadi (VETA) kilichojengwa na kanisa la Mission to Unreached Area Church (MUAC) lililopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
 Askofu mkuu wa kanisa la Mission to Unreached Area (MUAC),  Samwel Meena kulia akimpa maelezo mafupi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama wakati wa halfa ya ufunguzi wa chuo hicho cha VETA.
Askofu mkuu wa kanisa la Mission to Unreached Area (MUAC), Samwel Meena akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa chuo hicho cha ufundi stadi amabcho imejngwa kwa ajili ya kuweza kuwasaidia vijana wanaotoka katika maeneo ya vijiji.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...