Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefunga mafunzo kwa vikundi vya wajasiriamali vya wanawake na vijana manispaa ya Shinyanga yaliyolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia vizuri fedha za mikopo walizopewa na manispaa hiyo.

Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wanawake na vijana 60 kutoka vikundi 20 vya wajasiriamali ambao wamepata mikopo ya shilingi milioni 125.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo leo Jumatatu Machi 19,2018 Matiro aliwataka vijana na wanawake hao kutumia fedha walizopewa kwa malengo waliyokusudia na kuhakikisha wanaanzisha viwanda vidogo vitakavyoinua uchumi wao.

“Tumieni mikopo hii kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo ili kumuunga mkono rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli anayetaka Tanzania iwe nchi ya viwanda,pale mnapokwama tafadhali wasilianeni na viongozi wa serikali,tutawasaidia na pia tutatembelea miradi yenu ili tujue mnachofanya”,alisema Matiro.

Aidha aliwataka vijana na wanawake kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo kwenye halmashauri za wilaya ,mikopo ambayo haina masharti magumu wala riba kubwa ukilinganisha na taasisi za kifedha (benki).“Msikubali kukata tama kwamba maisha ni magumu,hata siku moja serikali haiwezi kugawa pesa kwa mtu mmoja mmoja,anzisheni vikundi vya ujasiriamali,kisha ombeni mikopo kwenye halmashauri,pesa zipo”,aliongeza Matiro.
Washiriki wa mafunzo kwa vikundi vya wajasiriamali vya wanawake na vijana  wa manispaa ya Shinyanga wakiwa wamesimama baada ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuingia ukumbini kwa ajili ya kufunga mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wanawake na vijana kutumia kwa malengo yaliyokusudiwa pesa za mikopo walizopata
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiimba wimbo kuhusu wanawake ...."Wanawake wote hongeraa...."

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...