MKUU wa Wilaya ya Kibaha Bi Assumpter Mshama amewaahidi kina mama wajasiriamali wa Wilaya ya Kibaha kuwa atazungumza na uongozi wa Halmashauri ya Mji ili itengwe siku na eneo maalum kwa ajili ya kufanya maonyesho ya bidhaa wanazozitengeneza ikiwa ni katika kupambana na changamoto ya ukosefu wa masoko ya kuuzia bidhaa hizo.
Mshama amesema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Kibaha Mkoa wa Pwani, amewataka wanawake kujiamini, kushikamana na kuachana na dhana potofu ya kupigana vita katika maeneo mbalimbali kwani adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe.
Aidha amesema kutokana na wanawake wengi kutofahamu sheria za ndoa na mirathi , talaka na sheria ya ardhi ya mwaka 1999, Halmashauri ya Kibaha itaendelea kutoka elimu ya sheria kwa kupitia wadau wa masuala ya sheria.
Amewataka wanawake wote nchini kuitafakari siku hii maalum kwa kutafakari mafanikio na changamoto na kuweka utatuzi wa changamoto wanazokabiliana nazo wanawake huku kauli mbiu ikisema kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe uswa wa jinsia na uwezeshaji wanawake vijijini kauli mbiu hii inahamasisha jamii kuongeza fursa za kiuchumi kwa wanawake ili kuwajengea uwezo katika nyanja zote za maendeleo, kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kitaaluma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...