Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

UAMUZI dhid ya pingamizi la awali lililowasilishwa na Jamuhuri katika Mahakama ya Rufaa kupinga maombi yaliyowasilishwa na mfanyabiashara James Rugemarila kupinga kukataliwa kupewa dhamana Mahakama kuu kujulikana hivi karibuni.

Jopo la majaji linaloongozwa na mwenyekiti, Bernad Luanda,Batueli MMimilla na Gerald Ndika limesema litatoa uamuzi tarehe itakayopangwa na pande zote mbili zitajulishwa.

Katika maombi hàyo, upande wa Jamuhuri unawakilishwa na Zainabu Mango,Peter Maugo na Tumain Kweka ambapo Rugemarila alijiwakilisha mwenyewe.

Katika maombi hayo Rugemarila anaiomba Mahakama ya Rufaa imruhusu kufanya mabadiliko ya taarifa ya kusudio la kukata rufaa.Pia anaomba kumuunganisha mshtakiwa mwenzake katika kesi ya Economic, Harbinder Seth kama mtu muhimu katika maombi hayo na anaomba wapatiwe dhamana wakati rufaa yao inaendelea kusikilizwa. 

Upande wa Jamuhuri uliwasilisha pingamizi la awali na kupinga maombi hayo kwa madai yameletwa chini ya kifungu kisicho sahihi.Kwani hakielekezi maombi hayo ni ya jinai au madai na kuiomba Mahakama iyatupilie mbali baada ya kusikiliza pingamizi hilo.

Mahakama imesema itawataarifu wahusika tarehe ya kutolewa kwa uamuzi huo.Baada ya kusema hayo Rugemarila aliiomba Mahakama itupilie mbali pingamizi la Jamuhuri kwasababu pingamizi hilo limeletwa kwa kanuni isiyo sahihi.Alidai pingamizi hilo halina ufafanuzi kuhusu sababu za pingamizi na kuiomba Mahakama itupilie mbali na ataeleza kwanini amemuunganisha Seth kama mtu muhimu.   

Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za kimarekani 22, 198,544.60 na Sh, bilion 309

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...