Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema inaendelea na utaratibu wa ukarabati wa shule kongwe nchini ikiwemo za sekondari na ufundi ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza masuala mbalimbali ya ubunifu kwa kutumia sayansi na teknolojia ya kisasa kulingana na mazingira yanavyobadilika .
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia elimu msingi, Dk.Avemaria Semakafu wakati alipokuwa akizungumzia kongamano la Siku ya Wanawake lililoandaliwa na Mfuko wa  Ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF).
Dk.Semakafu amesema ni vyema wakajirudisha kwenye mazingira yetu ya kitanzania kwa kuwafanya wasichana kuwa wabunifu kuanzia ngazi ya familia na shuleni ili kupata wasichana viongozi.
Amefafanua Shule za Sekondari Ifunda, Tanga, Mtwara na Moshi ambazo tangu awali zilikuwa zikitoa mafunzo ya ufundi, zinaendelea na ukarabati na wanatarajia mwaka wa masomo 2018,19 kuanza kidato cha kwanza.
 Naibu Kiongozi  Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF), Joseph Manirakiza akizungumza juu ya  kongamano hilo ili kutoa fursa kwa watu kujifunza namna wanawake wamefanikiwa katika masuala ya ubunifu na kuleta maendeleo katika jamii inayoiwazunguka.
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia elimu msingi, Dk Avemaria Semakafu  akizungumza katika kongamano la Siku ya Wanawake lililoandaliwa na Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)

 Mmoja wa watu waliokuwa katika uchangiaji mada aliekuwa mrembo wa Miss Tanzania na kutwa taji la urembo wa Afrika Nancy Sumari akizungumza jambo wakati wa kongamano la Wanawake lililoandaliwa na mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)
 Wadau mbalimbali waliofika katika Kongamano la Wanawake lililoandaliwa na Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF)
 Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka shirika la Dot Tanzania, Ndimbuni Msongole akizungumza jambo juu ya ubunifu kaytika nyanja ya mawasiliano wakati wa Kongamano la Wanawake na ubunifu lililoandaliwa na Mfuko wa  ubunifu wa Maendeleo ya watu kutoka nchini Uingereza (HDIF). Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...