Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanikiwa kumkamata mganga wa Jadi mwenye kupiga ramli chonganishi na kusababisha Mauaji ya mama mmoja aliyefahamika kwa jina la NDILU MBOGOSHI, Miaka 65, Msukuma, Mkulima, Mkazi wa Shilabela Kata ya Ulyankulu wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora, ambaye aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani. Mara baada ya tukio hilo upelelezi ulifanyika na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora liliweza kubaini na kumkamata mganga wa jadi huyo ambaye amefahamika kwa jina la THERESIA PAULO, 57YRS, MSUKUMA, mganga wa jadi na mkazi wa ISAGEGE-SASU Tarafa ya Ulyankulu wilaya ya Kaliua.
 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora SACP Wilbroad Mutafungwa akitoa taarifa za kukamatwa kwa Mganga wa Jadi anayepiga ramli chonganishi na kusababisha Mauaji.
Picha hapo juu: Mganga aliyekamatwa akiwa pamoja na vifaa vyake vya kazi ambaye anapiga ramli chonganishi iliyosababisha Mauaji huko Ulyankulu Mkoa wa Tabora.Picha na Habari toka kwa Omar Matesa @ RPC TABORA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...