Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT), Gaudentia Kabaka ametumia Siku ya Wanawake Duniani kuwapongeza wanawake wote nchini kwa kutekeleza majukumu yao wakiwamo wauguzi na madaktari wanawake wa Hospitali ya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.

Mbali ya kuwapongeza kwa kutekeleza majukumu yao, pia ameshiriki kufanya usafi wa mazingira na kisha kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni ishara ya upendo miongoni mwa wanawake wote nchini.

Akiwa hospitalini hiyo ya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam leo, amepata nafasi ya kusalimia wagonjwa waliokuwa wamelezwa na kutembelea akina mama ambao wamejifungua waliokuwa wadi ya wazazi.

Akizungumza hospitalini hapo amesema leo ni Siku ya Wanawake Duniani,hivyo UWT imeamua kuwatembelea kwa lengo la kuwapongeza kutokana na majukumu wanayoyafanya na wakati huohuo kusalimia wagonjwa na kutoa kidogo walichonacho kama ishara ya upendo.

"Niwapongeze wote kwa namna mnavyotekeleza majukumu yenu. Tuwapongeze kwa huduma nzuri ambazo mnazitoa kwa Watanzania wenzetu ambao wanaendelea kupatiwa matibabu."Tuendelee kudumisha upendo na mshikamano miongoni mwetu na hata kipande cha kanga ambacho tumetoa kwa baadhi ya akina mama si kitu kikubwa lakini ni kuthibitisha 

namna ambavyo UWT iko pamoja nanyi,"amesema Kabaka.Akiwa hapo Kabaka ameungana na viongozi wa ngazi mbalimbali wa UWT ngazi ya Wilaya na Mkoa kwa kufanya usafi wa mazingira ambapo kabla ya kuona wagonjwa waliamua kufagia eneo la hospitali hiyo.

Baadhi ya waguzi na madaktari wa hospitali hiyo wamemshukuru kwa kuonesha namna ambavyo UWT imeamua kuwatembelea na kushirikiana nao katika kufanya usafi na kutoa vifaa mbalimbali.
 Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka akifurahia mtoto wa kike, alipotembelea wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Mbaala Rangi tatu, wilayani Temeke Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani, leo Machi 8, 2018. Mapema Mama Kabaka akiambatana na kina mama mbalimbali wakiwemo viongozi wa UWT kutoka maeneo mbalimbali, alishiriki kufanya usafi na baadaye kutoa zawadi mbalimbali kwa uongozi na waonjwa kwenye Hospitali hiyo. Kulia ni Mariam Salum, mzazi wa mtoto huyo.
 "Wauuzi na Madaktari honereni kwa kazi nzuri na hasa kwa kujali afya za kina mama na watoto...endeleni kuchapa kazi tupo pamoja nanyi", alisema Mama Kabaka wakati akizunumza na baadhi ya wauguzi na madaktari wa hospitali ya Mbagala Ranitatu wakati wa ziara hiyo. Kushoto ni Matroni wa wodi ya Wazazi Maria Lumambo
 Diwani wa Viti Maalum CCM, Mariam Mtemvu na wenzake wakimsalimia mmoja wa Kina mama aliyekuwa katika Wodi ya Wazazi baada ya kujifungua katika hospitali ya Mbagala Ranitatu, leoPICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...